Mshambuliaji
 nyota Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa ameonekana akifanya mazoezi mara mbili, 
baada ya kumaliza awamu ya pamoja na wenzake Yanga SC chini ya kocha 
wake, Mholanzi Ernie Brandts akaenda katika ufukwe wa Coco kufanya 
mazoezi binafasi. 
Ngassa ambae ameanza kucheza juzi katika mechi kati ya Yanga na timu ya Ruvu Shooting ya RUVU, Mkoani Pwani baada ya kutumikia kifungo cha michezo 6 pamoja na kuilipa timu ya Simba pesa zake shilingi milioni 45 baada ya kuamuriwa kufanya hivyo na TFF ikiwa ni adhabu baada ya kuingia mkataba na Simba huku akijua kuwa bado ana mkataba na timu ya Azam.
Mchanganuo wa pesa hizo ni kwamba shilingi 30 milioni ni fungu alilolipwa na Simba na shilingi milioni 15 ni fidia. Mchezaji huyo alilazimika kulipa pesa hizo kutoka katika akaunti yake mwenyewe ambazo alilipa siku ya Ijumaa na siku ya Jumamosi alicheza mchezo kati ya Ruvu na Yanga ambapo timu yake ilipata ushindi wa bao 1-0 huku yeye akitoa pasi ya goli hilo kwa mfungaji Hamis Kiiza 'Diego'.
Katika hali ya kushangaza Ngassa ameomba wanachama na wapenzi wa Yanga walioguswa na 
kitendo cha kulazimika kujilipia mwenyewe fedha za Simba SC, Sh. Milioni
 45 kumchangia katika akaunti namba 01J2095037800 katika benki ya CRDB 
kwa jina la Mrisho Halfan Ngasa. “Naomba
 wanachama na wapenzi wa Yanga SC walioguswa kunichangia fedha katika 
akaunti hiyo ili tuwe tumesaidiana kulipa deni hilo,” alisema.
![]()  | 
| Ngassa akijifua peke yake Coco Beach | 
Ngassa alipoulizwa kuhusu
 kufanya mazoezi ya ziada, alisema ni kwa sababu pia anakabiliwa 
na kazi ya ziada kuisaidia timu yake katika Ligi Kuu, hivi sasa ikiwa 
inazidiwa na wapinzani wa jadi, Simba SC kwa pointi tano kileleni.  
Ngassa anadai Simba SC ilimwambia kuwa anasaini kucheza kwa mkopo kumalizia Mkataba wake wa Azam, lakini kumbe ni Mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo baada ya ule wa mkopo kumalizika.
“Nawashauri wachezaji wenzangu kwamba, wanapoingia mikataba na klabu, wahakikishe wanakuwa na mawakili, ili wawasaidie kujua kilichomo ndani yake na wasaini mikataba ambayo wanaielewa,”
Chanzo:http://tinyurl.com/k6td4pn








787857759.jpg)



































