Facebook Comments Box

Saturday, March 15, 2014

HUU NDIO MFANO WA KUIGWA ULIO ONESHWA NA VIONGOZI WA YANGA

Uongozi wa klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans umeonyesha mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa soka nchini siku moja baada ya kurudi kutoka Misri walipoenda na timu kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya  klabu hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi kwenye safari yao nchini Misri.

"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni 39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.


Saturday, March 1, 2014

PICHA: YANGA ILIPO INYONYOA AL AHLY

Young African Sports Club leo imefanya yale ambayo watanzania wengi walio tarajia baada ya kuinyonyoa Al ahly kwa bao moja kwa bila.
Bao lilifungwa na Nadir Haroub katika dakika ya 82.
Yanga ndio iliocheza mpira safi na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
Washabiki wengi wanasema kwa mpira walio onesha Yanga waarabu watatolewa na Yanga.

Tunawatakia Yanga kila la heri.
Chini ni picha za mpambano huo zikiwemo za washabiki wa Simba ambao waliamua kung'oa viti na kuwarushia washabiki wa Yanga.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU