![]()  | 
| Baada ya kutambulika rasmi na EWURA kama wasafirishaji halali wa abiria. Kamera yetu imeiona pikipiki maarufu kama bodaboda ikiwa na namba nyeupe za kibiashara. | 
Monday, March 4, 2013
BODABODA ZAANZA BIASHARA RASMI NA NAMBA ZA BIASHARA DAR ES SALAAM
UTATA WA KIFO CHA BENSON MOLLEL
![]()  | 
| Benson Mollel wa kwanza kushoto akiwa katika moja ya shughuli za UVCCM mkoani Arusha | 
 MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi 
(UVCCM) taifa, kupitia Mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) amekutwa 
amefariki dunia ndani ya Hoteli ya Lush Garden Business,  iliyopo Mtaa 
wa Jacaranda katikati ya Jiji la Arusha.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mollel alikutwa 
akiwa amekufa jana mchana na kwamba tukio hilo limezua hofu kwa wakazi 
wa Jiji la Arusha, huku wakijiuliza chanzo cha kifo chake.
Kifo cha mwanasiasa huyo mchanga ambaye pia 
alikuwa ni mfanyabiashara wa madini mkoani hapa, kimezusha maswali mengi
 wakati wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa na upande 
mwingine wakidai ni masuala la kibiashara.
Hisia hizo zinatokana na ukweli kwamba Arusha ni 
jiji lenye hekaheka za kisiasa hasa ndani ya CCM ambapo Mollel alikuwa 
mmoja wa vinara wake.
Polisi waliwasili hotelini hapo saa 8.00 mchana na
 kuupakia mwili wa marehemu kwenye gari na kisha kuupeleka Hospitali ya 
Mount Meru kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya wa Arusha (OCD), Gilles 
Muruta akizungumza katika eneo la tukio alisema: “Tunachunguza  tukio 
hili ambalo ni la ghafla.”
Akizungumzia kifo hicho, Katibu Mkuu wa UVCCM, 
Martin Shigela alisema: "Tumepokea kwa masikitiko kifo cha Mollel 
japokuwa sifahamu nini hasa kimejiri huko."
"Kuna rafiki yake alinipigia simu kuniarifu kuhusu
 kifo hicho na nikawaambia kama UVCCM Taifa tupate maelezo kamili na 
tujue nini cha kufanya. Iwapo familia itakuwa na mipango yoyote 
watutaarifu," alisema Shigela.
Baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wa madini 
mkoani Arusha walionekana nje ya hoteli hiyo baada ya taarifa za kifo 
hicho kusambaa na wengine walishindwa kujizuia kisha kuangua vilio.
Miongoni mwao ni kada wa Chadema, James ole Millya
 na diwani wa CCM Kata ya Mlangarini, Mathias Manga.  Katibu Mwenezi wa 
CCM wa Mkoa wa Arusha, Isaack Kadogoo ambaye pia alifika eneo hilo 
alisema kwamba wamepokea taarifa za tukio hilo kwa mshtuko mkubwa.
Uongozi wa hoteli hiyo haukuwa tayari kulizungumzia kwa madai kwamba limefikishwa katika vyombo vya usalama.
Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani 
ya hoteli hiyo vilidai marehemu aliwasili usiku, juzi Jumamosi hotelini 
hapo akiongozana na mwanamke aliyetambulika kwa jina la Nancy na 
kuchukua chumba namba 208.
SOURSE: MWANANCHI
Subscribe to:
Comments (Atom)




 

