Facebook Comments Box

Saturday, June 15, 2013

HUYU NDIO RAIS MPYA WA IRAN

Picture
Hassan Rouhani, Rais Mpya wa Iran
Kiongozi mwenye msimamo wa kati kutoka kwenye chama cha Wahafidhina nchini Iran, Hassan Rouhani, ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini humo.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran imesema, Rouhani ameshinda za zaidi ya kura millioni kumi na nane, ambayo ni zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.

Wizara hiyo imesema kuwa, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo walijitokeza kupiga kura kiwango ambacho kinakadiriwa kuwa asilimia sabini na tatu ya watu waliosajiliwa.

Mayor wa mji wa Tehran, Mohamad Baqar Qalibaf, alimaliza katika nafasi ya pili


BOMU LALIPUKA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA

Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu wamejitolea vyombo binafsi vya usafiri na wengine wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.

Bomu hilo linaelezwa kuwa lilipuka kwenye mkusanyiko wa watu meta chache kutoka jukwa kuu, mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo hilo.

Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. Mwandishi mmoja wa habari anaripotiwa kunyang’anywa kamera yake baada kwa kupiga picha, hata baada ya kujitambulisha.

Watu wenye hasira wanaripotiwa kuyashambulia na kuyaharibu baadhi ya magari ya kutoa huduma ya kwanza (ambulance) kwa kuwa yalichelewa kufika kuwaokoa majeruhi.

ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa  hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye kitufye cha kuelekea mbele



SIKILIZA MAHOJIANO YA MAREHEMU LANGA KILEO NA DR. ISAAC MARO WA CLOUDS FM

www.kitongoni.blogspot.com
Langa Kileo



KIBONZO: JINSI YA KUKUMBUKA NENO LA SIRI




ANGALIA VIDEO ZA SHOW YA LADY JAY DEE NA MWANA FA ILI UJUE NANI KAMFUNIKA MWENZAKE



Komando Jide akifanya vitu vyake jukwaani



Hapa Fa akiongea



Hapa Fa akiimba unanitega



Hapa Fa akiimba yalaiti

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU