Facebook Comments Box

Saturday, September 21, 2013

HIGHLIGHT: CHELSEA 2 - 0 FULHAM ANGALIA MAGOLI HAPA




MBEYA CITY YAENDELEA KUTESA VIGOGO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA


Mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe akimtoka beki wa Mbeya City Anthony Matogolo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo. Timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.  
 
Timu ya Mbeya City imetoka sare kama kawaida yake katika uwanja wa Taifa leo ilipokuwa inacheza na Timu mwenyeji wa uwanja huo Simba SC ya Msimbazi Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo jioni. 

Simba ambayo hata baada ya sare hiyo inaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo baada ya kufikisha alama 11 kibindoni huku Mbeya City ikifikisha alama 7 baada ya michezo mitano iliyocheza.

Simba ndiyo ilikuwa yakwanza kupata bao katika dakika ya 29 kupitia kwa mshambuliaji wake hatari kutoka Burundi Amis Tambwe aliyepokea pasi kutoka kwa Haruna Chanongo na baadae kuongeza bao lingine katika dakika ya 33 kwa shuti kali baada ya pasi kutoka kwa Betram Mombeki, Tambwe aliwadhihirishia mashabiki wa timu hiyo na timu pinzani kuwa hakubahatisha kufunga Hat Trick katika mechi iyopita dhidi ya Mgambo Shooting ya Tanga iliyochapwa bao 6 kwa Ubuyu na Simba.

Mbeya City, timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi ilijipatia bao katika kila kipindi ambapo bao lake la kwanza lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 37 kwa shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Simba Abbel Dhaira, wakati la kusawazisha lilifungwa na Richard Peter dakika ya 69 akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Mwigane Yeya.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, Charles Mbilinyi na Juma Mwita wa Mwanza, Simba SC inafundishwa na mshambuliaji wake wa zamani, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’,

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Kaze Gilbert/Hassan Hatibu dk66, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha Ibrahim/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk50, Amri Kiemba/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk79, Betram Mombeki, Amisi Tambwe na Haroun Chanongo. 

Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Antony Matogolo, Yohana Morris, Mwigane Yeya/Richard Peter dk59, Steven Mazanda, Paul Nonga, Deus Kaseke na Yussuf Willson.   

Katika mechi nyingine, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Mgambo Shooting Stars wametoka sare ya 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora, Prisons imetoka 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya, wakati Kagera Sugar imeshinda 3-0 dhidi ya Ashanti United ya Dar es Salaam Uwanja wa Kaitaba.

Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wake wa tano kesho kwa mechi tatu ambazo ni Azam na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex na mechi kati ya Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.


SHAMBULIO LA NAIROBI LAUA WATU KADHAA


Scramble: People rush for safety away from gunfire between police and armed attackers

Relief: A woman who had been held hostage makes it out alive from the mall

Fleeing: A child runs to safety across the shopping mall
Devastating: Injured people receive assistance from bypassers at the scene of the shooting
Search: Police scour the centre with guns to try and locate the terrorists still holding hostages

Rescue: A woman is shipped to an ambulance in a shopping trolley by centre staff
Safety: Shoppers and shop assistants raise their hands as they are escorted out by armed police

Killings: At least 15 people are believed to be dead, although police have not confirmed a death toll
Victim: Rescuers attempt to evacuate a man injured in a shootout

Horror: Customers are evacuated from the shopping centre covered in blood
Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti pia yalitumika, Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.

Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machela.

Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo. Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika pia.


DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI


Daktari@ @
DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
 
‘Daktari’ huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno. Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.

Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari .

Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.

Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.

Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.

Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.

Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.

Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali. Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.

Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.

Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.

Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.

Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.

“Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi,” alisema.

Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa ‘Masters of Medicine’, ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.

Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.

Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi;- Habari leo


AGNES MASOGANGE AACHIWA HURU


Agnes Gerald maarufu kama Masogange

Johannesburg. Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo, Mahakama ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye. Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.
Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.

Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.
“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu,” alisema Muller kwa kujiamini.
Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.
“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema Nzowa.
Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.
“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema Nzowa.
Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.
“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini,” alisema.
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi. Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.
Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani. Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege. Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.
Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini.

CHANZO: MWANANCHI



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU