  | 
| Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wakipita jirani na unapojengwa mmoja
 wa mitambo wa kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi, Jijini Dar es 
Salaam, walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupokea gesi.  | 
  | 
| Pichani
 ni mmoja wa Mtambo wa kuzalisha umeme ambao ni miongoni mwa mitambo 
itakayotumiwa katika kuzalisha kiasi cha megawati 150 za umeme katika 
Mradi wa Kinyerezi I. | 
 
  | 
| Meneja
 Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi, Saimoni akiuleza jambo 
ujumbe wa Washirika wa Maendeleo  wakati walipotembelea kuona maendeleo 
wa ujenzi wa mradi huo. | 
 
  | 
| Katibu Mkuu
 Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, akiwaongoza Washirika wa 
Maendelo kuangalia namna utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha 
Kuzalisha Umeme na kituo cha kupokea Gesi unavyoendelea katika eneo la 
Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni mojawapo ya mapipa 
yatakayotumika kuhifadhi mafuta ambayo yatatumika wakati wa dharura. | 
Washirika
 wa Maendeleo kutoka taasisi mbalimbali nchini waliotembelea Mradi wa 
kuzalisha Umeme  wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi  wameeleza 
kufurahishwa na kuridhika na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Mkurugenzi
 Mkaazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Uganda na 
Burundi, Philippe Dongier, akiongea kwa niaba ya washirika hao ameeleza 
kuwa, wameridhishwa na hatua ambazo miradi hiyo imefikia na kupongeza 
jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba inafanyia kazi changamoto ya 
upatikanaji umeme wa uhakika Tanzania. Pia Dongier ameitaka Serikali 
kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme ili 
iweze kufikia lengo lake la kuhakikisha Tanzania inazalisha umeme wa 
kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza
 wakati ujumbe huo ulipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa kiasi cha 
megawati 150 na  kituo cha kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi jijini 
Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim 
 ameeleza kuwa, Wizara imeona ni jambo la msingi kwa wadau hao 
kutembelea miradi hiyo ili kujionea hatua mbalimbali ambayo miradi hiyo 
imefikia.
Aidha, Maswi ameongeza kuwa, 
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imedhamiria kuleta 
mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya nishati hususani kupitia gesi 
asilia na kuongeza kuwa, hakuna kinachoshindikana hivyo, miradi hiyo 
inatarajiwa kukamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa.
Kwa
 mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la 
maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba, ameeleza
 kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea gesi cha Dar es Salaam umekamilika 
kwa asilimia 60. Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha 
Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
 Mhandisi, Saimoni Jilima ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 70.Washirika
 wa Maendeleo  waliotembelea miradi hiyo ni pamoja na  Benki ya Dunia, 
GIZ, USAID, MCC, Korea Exim Bank, Benki ya Maendeleo ya 
Afrika(ADB),DFID, Umoja wa Ulaya,Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Norway, 
Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Ufaransa