Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakimpa kichapo mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango, nje ya Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe 
akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano 
Mkuu wa chama hicho hivi karibuni, kuwa watafanya maandamano nchini nzima
 bila kikomo, lakini mwenyekiti huyo aliachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano yaliyochukuwa muda wa saa tano.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa 
Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la 
Polisi mapema leo.

Ulinzi mkali wa Polisi kama wanavyo onekana.

Ondokeni, Polisi akiwataka wanachama wa Chadema kuondoka eneo hilo kwani hawahusiki.
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari 
Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa 
kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe 
alihojiwa na Polisi kwa muda wa saa tano na baadae alichiwa kwa dhamana.

