Kamati ya Sheria, Maadili na 
Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia maombi ya 
usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi 
Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia 
timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wengine 
waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni 
Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah 
Seif, Malika Ndeule na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, 
Njaidi Mohamed na Mahmoud Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed kayi na 
Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin Selemani, Shaibu Nayopa,
 Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami Mnyangamala, 
Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim, Chacha 
Marwa, Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward
 Mzeru na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius 
Mrope (Kagera Sugar).
Rajab Mohamed, Zakayo Joseph, 
Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro Pazi- kwa mkopo, 
Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT Ruvu), 
Moaka Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald 
Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto 
Africans).
Obadi Mungusa, Juma Seif, Yusuf
 Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa mkopo, Buya Jamwaka, 
Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, 
Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel 
Dhaila (Simba).
Rashid Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji Martin Mlolere 
aliyeombewa usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji amekataliwa kwa vile
 taratibu za uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya 
Majimaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
T.F.F
