
 Hip hop inauza kwa mujibu wa Hamisi Mwinjuma au Mwana 
FA kama anavyo fahamika kimuziki ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi 
karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza 
miito ya simu yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Mwana FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.