Mkurugenzi Mkuu wa 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), Felix Ngamlagosi
 (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini 
kwake Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta nchini na 
katika soko la Dunia. Kulia ni Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel.
 Mkurugenzi wa Petroli, Godwin Samwel (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti 
wa Nishati, Maji na Mafuta (Ewura), imepunguza bei za mafuta kote nchini
 kuanzia leo kutokana na kudorora kwa uchumi wa bara la ulaya.
Hayo yalibainishwa 
 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta 
(Ewura), Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na waandishi wa habari 
ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mwenendo wa bei za mafuta
 nchini na katika soko la Dunia.
Alisema kuanzia leo 
bei ya mafuta ya petroli kwa lita moja itauzwa sh.1955 na hiyo inatokana
 na kushuka kwa jumla ya asilimia 16 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.311
 kwa lita.
 Alisema bei ya 
petroli katika soko la dunia imeshuka kwa jumla ya aasilimia 25 kuanzia 
Julai hadi Novemba 2014, sawa na pungufu kwa jumla ya dila 249 kwa tani.
Ngamlagosi alisema 
mafuta ya dizeli kwa lita moja yatauzwa sh.1846 na kuwa bei hiyo 
imeshuka kwa asilimia 13 sawa na pungufu kwa jumla ya sh.244 kwa lita na
 kuwa dizeli kwa soko la dunia imeshuka kwa jumla ya asilimia 28 kuanzia
 Julai hadi Novemba 2014 sawa na pungufu kwa jumla ya dola 189 kwa tani 
na kuwa mafuta ya taa yatauzwa sh. sh.1833 kwa lita.
Alisema katika 
kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 
2014, bei za mafuta ghafi zimekuwa zikishuka kwa kasi ikilinganishwa na 
kipindi cha hapo nyuma ambapo zimeshuka toka dola 100 kwa pipa hadi 
kufikia wastani wa dola 60 kwa pipa moja ambayo ni sawa na  karibu 
asilimia 40.
Alisema viwango hivyo
 vya bei iliyopungua ni katika soko la Dar es Salaam na mikoa mingine 
bei zao zimepangwa kutokana na kuwepo kwa gharama za usafirishaji.
Ngamlagosi alitoa 
mwito kwa wanunuaji wa mafuta hayo kuhakikisha wanapatiwa lisiti baada 
ya kununua kwani itasaidia kuwabaini wafanyabiashara wasio waaminifu 
ambao wataendelea kuuza kwa bei ya zamani.
"Natioa mwito wa 
kuwaomba wanunuaji wa mafuta kuhakikisha wanapewa lisiti kwani 
itatusaidia kuwabaini wale wanauza kwa bei ya juu, na pia itamsaidia 
mnunuzi iwapo atauziwa mafuta yaliyochini ya kiwango na ukusanyaji wa 
kodi ya serikali" alisema Ngamlagosi.
Naye Mkurugenzi wa 
Petroli, Edwin Samwel alisema Ewura imejipanga vizuri kuhakikishha 
hakuna ujanja ujanja utakaojitokeza wa kudai mafuta yamekwisha au 
yaliyopo yatauzwa kwa bei yaliyonunuliwa.
Alisema 
mfanyabiashara yeyote atakayekiuka utaratibu huo atachukuliwa sheria 
pamoja na kufungiwa biashara yake ingawa alisema hali hiyo 
haitajitokeza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)