Mbunge
 wa chambani (CUF) Visiwani zanzibar Salim Hemed Hamisi ameanguka ghafla
 akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa 
kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam wakati kamati
 hiyo ikiendelea na kikao chake
Mbunge 
huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya 
afya yake amefikwa na dhahama hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa 
kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha 
mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na 
matibabu zaidi.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Edward Lowasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
