
Vituko
 mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja 
kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16 
mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na 
hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi 
 kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu 
huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake 
mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa 
mshindo.
Baada
 ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na 
kuingia ndani na  ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake  
mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali 
kutoka kwa mama yake  mdogo.
Katika
 kipigo hicho Zawadi  alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa 
mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake 
Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia 
hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog