Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw.Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.
Afisa
 Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru 
wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango 
wa         TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani 
alipotembelea Nchini Tanzania.
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.
 Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Kampuni
 ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa Marekani kwa huduma 
bora iliyotoa  wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa nchini.
Akitoa
 shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka  ubalozi wa Marekani hapa 
nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania 
umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora na za uhakika  kutoka TTCL wakati 
wote wa ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza
 kuwa huduma walizozipata  zimethibitishwa na taarifa kutoka ofisi 
inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi walizopita 
Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya kiwango 
cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya 
Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Katika
 Shukurani zake Bw. Jeff Shrader alioa pia zawadi kwa Afisa Mtendaji 
Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura  na kwa baadhi ya wawakilishi kutoa 
fani mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa 
TTCL kama ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
