Facebook Comments Box

Tuesday, June 18, 2013

TAHADHARI: UGONJWA WA 'DENGUE' WAINGIA JIJINI DAR ES SALAAM


Kwa wale wafuatiliaji wa habari za magazetini, mtakuwa mmesikia kuhusu kuzuka kwa ugojwa uitwao "Dengue fever" ama kwa kiswahili huitwa Homa ya Dengue.

Habari zinasema kwamba tayari watu ishirini wameshathibitika kuwa na tatizo hili na tayari wako hospitali. Juma lililopita, ugonjwa huu uliua watoto wapatao 6 katika Wilaya ya Ilala na ikasemekana kwamba ni 'Malaria kali' lakini baada ya sampuli za damu kupimwa zaidi ilionekana walikuwa na homa ya dengue!

Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum. Na mbu hawa hupatikana kwenye Maji masafi yaliyoachwa wazi hivyo wananchi mnatahadharishwa kuhakikisha maji masafi yanafunikwa ili kuepuka mazalio ya Mbu hao.

Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida

  • homa kali zaid ya 40 degrees
  • maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
  • maumivu ya viungo na misuli
  • harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu

TIBA:

HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.

Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol. Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi. 
kwa mgonjwa ambaye ana shock yani kutetemeka au ana hali mbaya sana basi ni bora awahi hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha yake.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU