Kwa wale wafuatiliaji wa habari za magazetini, mtakuwa mmesikia
kuhusu kuzuka kwa ugojwa uitwao "Dengue fever" ama kwa kiswahili huitwa
Homa ya Dengue.
Habari zinasema kwamba tayari watu ishirini wameshathibitika kuwa na tatizo
hili na tayari wako hospitali. Juma lililopita, ugonjwa huu uliua watoto
wapatao 6 katika Wilaya ya Ilala na ikasemekana kwamba ni 'Malaria
kali' lakini baada ya sampuli za damu kupimwa zaidi ilionekana walikuwa
na homa ya dengue!
Ugonjwa huu huenezwa na Mbu aina ya aedes mosquito, na hawa mbu
wamegawanyika makundi 2 hivi, nafikiri watu wa taxonomy wataweza
kunisaidia vizuri zaid, na specifically mbu hawa hubeba vijidudu
viitwavyo dengue virus. Vijidudu hivi huwa na selflimiting kama walivyo
virus wengine hivyo jinsi ya kupona hakuna dawa maalum. Na mbu hawa hupatikana kwenye Maji masafi yaliyoachwa wazi hivyo wananchi mnatahadharishwa kuhakikisha maji masafi yanafunikwa ili kuepuka mazalio ya Mbu hao.
Dalili za ugonjwa huu
Dalili huanza kuonekana siku 4-7 baada ya kuumwa na mbu mwenye hawa virus.Dalili za dengue ya kawaida
- homa kali zaid ya 40 degrees
- maumivu makali ya kichwa na hasa kipanda uso
- maumivu ya viungo na misuli
- harara mwili mzima ambazo hutokea baada ya siku 3-4 baada ya kuumwa na mbu
TIBA:
HAKUNA TIBA MAALUM AMA KAMILI KWENYE HUU UGONJWA KAMA ILIVYO KWA BAADHI YA MAGONJWA YASABABISHWAYO NA VIRUSI.
Lakini mgonjwa anatakiwa apate muda wa kupumzika, anywe fluids kwa wingi na ameze dawa za kushusha homa hasa paracetamol.
Asprin haziruhusiwi kabisa kutumiwa unapoona dalili hizi.
kwa mgonjwa ambaye ana shock yani kutetemeka au ana hali mbaya sana
basi ni bora awahi hospitali na hapo atapatiwa matibabu ya haraka na
kumwongezea electrolytes ili kuokoa maisha yake.