MSANII
 wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady 
Jaydee (Pichani) muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka 
katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi
 wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.
Jaydee
 ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la
 wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa 
hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na 
kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.
Kikubwa
 ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni 
kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo.
Kati ya vielelezo alivyopewa
 na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na 
nakala za magazeti na nakala za Post za blog yake pamoja na tweets! 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog