Jeneza la bibi likielekea msikitini kwa ajili ya kuswaliwa 
   
Jeneza lenye Mwili wa Msanii mkongwe wa Muziki wa  Taarab, Marehem Fatma
 Bint Baraka Khamis(Bi Kidude) likitolewa katika msikiti wa Mwembeshauri
 aliposwaliwa mchana wa leo kabla ya kwenda kuzikwa. 
 
 Taratibu za Mazishi zikiendelea kama inavyo onekana katika picha 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein 
akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma
 Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa 
Kusini Unguja.   
  Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akiweka udongo 
katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi 
Kidude) Katika makaburi ya Kitumba wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo  
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq akiweka udongo.  
 |