Katika dirisha lile la treni,ndani yake
  Alikuwa kakaa mzee mmoja na kijana wake,
  Ambaye alikuwa na makamu ya umri wa miaka 25.
 
  Yule kijana akaanza kuonesha usoni mwake 
  alaza za furaha na mshangao. 
  Akatoa mkono wake dirishani,kisha akaurudisha
  Haraka na kusema kwa sauti ya juu:
  Baba angalia miti yote yakimbia kurudi nyuma!!
 
  Yule mzee akatabasamu na kuonesha ya kwamba
  Anaungana na mwanae katika furaha.
 
  Kando yao walikuwa wamekaa wanandoa wawili.
  Na wakisikiliza mazungumzo kati ya baba na mtoto.
  Wakawa wakihisi aibu na kushikwa na mshangao,
  Vipi kijana huyu mwenye makamo ya umri wa miaka 25
  Anafanya vitendo kama vya mtoto mdogo???
 
  Ghafla yule kijana akapiga kelele akisema:
  Baba angalia umeme wa radi!
  Angalia mawingu yanakwenda pamoja na treni!
 
  Wanandoa wawili wakaendelea kushangaa!
  Kulingana na mazungumzo na vitendo 
  Vya yule kijana.
 
  Kisha mvua ikaanza kunyesha,na matone ya maji
  Yakatua katika mkono wa yule kijana,ambaye 
  Alikuwa akionesha alama ya furaha katika uso wake.
 
  Akapiga kelele kwa mara nyingine na kusema:
  Baba mvua inavyesha !!! Na maji yamegusa mkono wangu !!!
  Baba angalia !!!
 
  Mara hii wanandoa walishindwa kujizuia,
  Wakamuuliza yule mzee:
  Mzee kwa nini humpeleki kijana wako hospitalini,
  Ili aweze pata matibabu???
 
  Yule mzee akawajibu:
  Hivi sasa ndio twatoka hospitalini,
  Na mwanangu ndio ameanza kuona kwa 
  Mara ya kwanza katika maisha yake.
  ******************************
 
  Siku zote usiwe ni mwenye kutoa 
  Majibu ya mambo mpaka ujue uhakika wake.
  Na daima uwe ni mwenye dhana nzuri
  Kwa ndugu zako.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog