Facebook Comments Box

Wednesday, August 3, 2016

TV 1 KURUSHA MECHI ZOTE ZA LIGI YA UINGEREZA

Kituo cha Televisheni nchini, TV1 leo hii kimezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la Toroka Uje ambayo inawaletea watazamaji wake matangazo ya bure ya mechi zote za Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League zitakazoanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 13 mwaka huu.
Akizungumzia kampeni hiyo Meneja Mkuu wa TV1,  Joseph Sayi alisema kuwa Watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuangalia ligi hiyo maarufu duniani lakini kupitia TV1 ambayo inapatikana kwenye king’amuzi cha Startimes, Watanzania watakuwa wakitazama mechi hizo bure bila gharama yoyote.

Naye Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu aliongeza kuwa mbali na watazamaji wa TV1 kufurahia mechi hizo ambazo zitarushwa kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho wa ligi, pia wamejiandaa kukutana na watazamaji wa TV1 kupitia michezo mbalimbali, matamasha na mashindano yatakayokuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo vifurushi vya king’amuzi cha Startimes na nyingine kibao.

Akizungumzia kuhusu kampeni hiyo ya Toroka Uje, Mkuu wa Uzalishaji vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo, alisema kuwa  kipindi hicho kitakachoanza kuruka tarehe 10 mwezi huu kitakuwa katika siku tatu ambapo kutakuwa na mijadala ya kandanda, mpira laivu na uchambuzi kuhusu mechi zijazo ambapo uchambuzi huo utaongozwa na wachambuzi wakubwa akiwemo Dr Leaky Abdallah na Ally Kashushu.

Aidha Meneja Masoko wa Startimes, Damien Li aliwahakikisha Watanzania kuwa Startimes haitaongeza bei ya vifurushi wala kutoza chochote kwa watazamaji wa Ligi hiyo kupitia TV1 kwa kuwa ni bure kabisa.


TETESI ZA USAJILI ULAYA


Chelsea wako tayari kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Loic Remy, 29, pamoja na dau litakaloweka rekodi Uingereza kitita cha paundi millioni 65 kwa mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 23. (Chanzo Daily Mail)

Everton wamekuwa waking’ang’ania wapewe paundi millioni 75 kwa mchezaji huyo pekee ambaye walimsajili kutoka Chelsea kwa paundi millioni 28 miaka miwili iliyopita. (Chanzo Sun)

Lukaku anafikiria kutoa ombi rasmi ili kulazimisha arudi tena Stamford Bridge. (Chanzo London Evening Standard)

Winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 25, amekubali kuhamia Arsenal, hii ni kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka nchini Algeria. (Chanzo Le Buteur)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kufikia muafaka juu ya dili la paundi millioni 50 la uhamisho wa beki John Stones, ambaye ndiye lengo lake kuu, ingawa Everton wamesisitiza kuwa bado kuna 'gepu kubwa' kati ya klabu hizo mbili juu ya ada ya uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Chanzo Daily Mirror)

Real Madrid inaweza ikawapa ofa Newcastle ya wachezaji wawili vijana - pengine Mariano Diaz, 23, na Marcos Llorente, 21 – kwa mikopo wa muda mrefu ikiwa ni kama sehemu ya mpango wa kumchukua kiungo wa Ufaransa Moussa Sissoko, 26. (Chanzo Guardian)

Stoke City wanafikiria kumtoa aidha Joselu, 26, Mame Diouf, 28, au Peter Crouch, 35, ikiwa West Bromwich Albion watataka wapewe mchezaji wa kubadilishana kwenye dili la uhamisho wa Saido Berahino, 22. (Chanzo Stoke Sentinel)

Paris St-Germain wamekubali kuwalipa Real Madrid yuro millioni 25 kama ada ya kumsajili winga Jese Rodriguez, 23. (Chanzo Marca)

Bastian Schweinsteiger ameambiwa atapewa nafasi ya kurudi Bayern Munich ikiwa ataondoka Manchester United. (Chanzo Sky Sports)



HUU NDIO USAJILI KAMI LI WA RUVU SHOOTING

Timu ya soka ya Ruvu Shooting, imekamilisha usajili wa wachezaji wake watakaoichezea msimu mpya wa 2016/17.

Wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, timu walizotoka kwenye mabano ni Jabir Aziz (Mwadui FC),   Richard Peter (Mbeya city), Elias Emanuel (Polisi Morogoro), Clidel Loita (Mji Njombe), Chande Magoja na Fuluzuru Maganga wote kutoka Mgambo JKT, Shaibu Nayopa (Oljoro), Abrahaman Musa (JKT Ruvu) na Renatus Kisasa ambaye ni mchezaji huru.

Aidha wachezaji wazamani walioachwa ni Ally Khan, Yahya Tumbo, Chagu Chagula, Juma Mpakala, Rashid Gumbo, Kulwa Mobi, Gidion Seppo na George Osei.

Timu iko kambini Mabatini ikiendelea na mazoezi ambapo Agost 1, ilicheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mbeya city na kupata ushindi wa bao 1-0, leo Jumatano Agost 3 itakuwa uwanja wa Polisi College, Dar es salaam kucheza na Polisi Dar es salaam ambapo Jumamosi ijayo itakuwa Mabatini ikipambana na Azam fc.

Imetolewa na;
Masau Bwire 
Afisa Habari na mawasiliano Ruvu Shooting.


Tuesday, August 2, 2016

YANGA NAO KUFANYA MKUTANO NA KUCHEZA MECHI YA KUJIPIMA

Baada ya watani wao kufanya mkutano wa mabadiliko nao Young African Sports Club wameitisha mkutano mkubwa tarehe 06 mwezi wa nane. Pamoja na mkutano huo itapigwa mechi kubwa ya kujipima nguvu kati ya Yanga na Mtibwa sugar kutoka turiani manungu Morogoro.

Chini ni taarifa ya mkutano huo.


SIMBA WAMUOMBA MO KUTIMIZA AHADI YAKE

Chini ni barua ya Simba kwenda kwa mkurugenzi wa Mohamed Interprises Kumuoomba asaidie usajili katika kutimiza ahadi yake baada ya wanachama kuridhia mabadiliko.


MAONI YA ZITTO KUHUSU MO SIMBA

Mwanachama wa Simba Zitto Zubery Kabwe nae amejitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kutoa maoni yake kuhusu mabadiliko yanayo elekea kufanyika Simba. Hapo chini ni maoni yake kuhusu mgawanyo wa hisa. 

20bn tshs endowment fund for Simba SC ni moja ya pendekezo bora zaidi kutolewa na Mwanamichezo nchini kwetu. Mohamed Dewji anapendekeza kuwa yeye atatoa tshs 20bn na kuziweka kwenye Endowment Fund kisha riba kutumika kuendesha Club. Tutakuwa na club matata sana nchini. Vyuo vikuu vikubwa duniani Kama Harvard vinaendeshwa kwa Mfumo huu anao pendekeza MO. Tukiwa na usimamizi mzuri wa Fedha tutakuwa timu bora kabisa na tutaweza hata kuwa na academy ya Simba Kama ilivyo kwa club kubwa duniani. 

Hata hivyo, nashauri kwenye muundo wa umiliki, mtu mmoja asiwe na Hisa zaidi ya 40%. Ushauri wangu ni mgawanyo ufuatao; 

- Mwekezaji ( MO ) 40% ( mkataba wake wa uwekezaji uonyeshe kuwa kwa kupewa Hisa hizi atafungua endowment fund ya thamani ya tshs 20bn na atakuwa na uhuru wa kuteua trustees wa Fund hiyo. Mwekezaji atakuwa na uhuru wa kuifunga fund iwapo asiporidhishwa na matumizi Fedha zinazotokana na Endowment Fund ). 

-  Wanachama wote wa Simba wagawiwe sawa 40% ( kuwe na cut off ya siku ya mwisho Mwanachama kujiunga kuweza kufaidika na kugawiwa Hisa hizo. Hisa za Simba SC zikishaorodheshwa kwenye soko la Hisa, Mwanachama atakuwa na uhuru wa kuuza Hisa zake freely. 

- 20% ya Hisa ziorodheshwe kwenye Soko la Hisa la Dar Es Salaam kwa ajili ya 1) kuvutia wawekezaji wengine 2) kukuza mtaji wa Kampuni 3) kuwezesha uwazi kwenye uendeshaji wa kampuni kwani Wanachama wote watakuwa wanajua kila kinachoendelea kwenye kampuni na club kwa sababu soko la Hisa Lina ' disclosure rules '. 

Kwanini MO asiwe na 51%? Sio MO tu, Memarts za Simba ziwe wazi kwamba hakuna mtu mmoja au kampuni moja au taasisi yeyote moja itakayoruhusiwa kuwa na zaidi ya 40% ya Hisa za kampuni. Hii itamfanya MO au mwekezaji mwingine yeyote kuhakikisha anatafuta 11% zaidi ili kupitisha maamuzi. Kuna hatari ya kumpa mtu mmoja uwezo wa kufanya maamuzi peke yake. Lazima kumfanya ashawishi japo 11% ya wenye Hisa ili kuboresha maamuzi. Leo ni MO anaipenda Simba, kesho unaweza kuwa na mtu asiye MO. Nadhani 40% ni kiwango cha kutosha kwa Mwekezaji. 

Nashauri wana Simba tusicheleweshe haya MABADILIKO. Tufanye sasa hivi ili msimu huu unaoanza tuwe na timu imara yenye uhakika wa kushiriki Premier League. Mpango wa MO wa Endowment Fund ni Mpango bora na tusipoteze nafasi hii.


Saturday, May 14, 2016

JPM AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIPORT

 Raisi Magufuli akipata maelezo toka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa pembeni akisikiliza kwa makini.
Kushoto ni mashine ambaye imekuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu ambayo imeliingizia Taifa hasara kwa kupitisha mizigo bila kukaguliwa kutokana na ubovu wake. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jana tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.

“Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili."Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege

“Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogondogo napita tu” Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere



SOMA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YALEO JUMAMOSI TAREHE 14-MEI-2016 HAPA

Read more...

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU