Kushoto ni mashine ambaye imekuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu ambayo imeliingizia Taifa hasara kwa kupitisha mizigo bila kukaguliwa kutokana na ubovu wake. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na 
Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja 
dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo
 na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es salaam.
Rais
 Magufuli ametoa agizo hilo jana tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya 
kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za 
sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.
Maafisa
 wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa 
wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria 
katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu 
utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli 
aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola 
kuchukua hatua mara moja.
“Unajua
 mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini 
nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, 
ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio 
mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu 
mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi 
miwili."Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege
“Kwa
 hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa 
hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu 
zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege 
ndogondogo napita tu” Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog


