Facebook Comments Box

Friday, August 29, 2014

UNANYASAJI MTANDAONI UMEMUUWA BETTY NDEJEMBI : TUPINGE UNYANYASAJI MITANDAONI

Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine.Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: "kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli Kamwe asilani".

Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.

Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na
kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala
zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.

Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye
'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo,
utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'

Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye
mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya
kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.

La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki
kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa
wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha
suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali
ya utani japo wenye ukweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa
kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.

Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa
binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali Hata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu.

Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za
marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na
wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni
maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu
hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.

Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa
'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa burried kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila
aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.'

Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana
yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi
ku-RT upuuzi.

Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu
unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma
vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya
'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi. Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako.

Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa
wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu
ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno
macha Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.

Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao. Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu. Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.

Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa
udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu
ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.

Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi
gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.

Chanzo: Vijimambo Blog


MAKUNDI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE




BAADA YA KUWA NA MGOGORO NA YANGA OKWI RASMI SIMBA

NA BIN ZUBERY

STAILI ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emannuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inatumia kumrejesha kundini Mganda huyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam,
Okwi amesema kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye
jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki
ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa
kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC,
Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji.

“Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi
hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.




MAGAZETI YA LEO: IJUMAA TAREHE 29/08/2014






Thursday, August 28, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA PROGRAMU YA UIMARISHAJI MIPAKA YA KIMATAIFA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka. (picha hii na zote zinazofuata ni kutoka Ikulu)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakitembelea eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakitembelea eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipata maelezo na kuangalia vifaa vya upimaji eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizindua kwa pamoja eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipongezana kwa furaha katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakichanganjya udongo na kujenga kwa pamoja alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakichanganjya udongo na kujenga kwa pamoja alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na wananchi wa nchi zao wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Burundi na Tanzania zikipigwa katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakijipatia chakula cha mchana katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiagana katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.





VIDEO: HIGHLIGHTS - ARSANAL vs BESIKTAS 1-0



VIDEO: VICTORIA KIMANI FT DIAMOND AND OMMY DIMPOZ - PROTOKO



MAGAZETI YA LEO: TAREHE 28/08/2014 ALHAMISI













ASKARI WAWILI MBARONI KWA KUJERUHI

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela

--------------------------------------------------
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili
kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki
aliyejulikana kwa jina la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma
mjini Songea.
Akizungumza kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msekhela amesema tukio hilo limetokea Agosti 26 mwaka huu
majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea
ambapo askari polisi wawili PC Waziri mwenye namba G 5075 na
PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria na piki piki ya
polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina ya Yamaha CC 250
katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki huyo
kwa kumpiga risasi.
Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi
na askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo
iliyokuwa imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye
alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na
mwendesha piki piki aliyejulikans kwa jina moja la Agrey ambaye
alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa piki piki iliyokamatwa na askari
hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.
Ameitaja piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni
aina ya San Lug yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada
ya mwendesha piki piki huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini
wake Agrey alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa
waendesha piki piki maarufu kama Yebo yebo ambao walianza
kuwarushia mawe askari hao huku majeruhi akiwa ameshika mtutu
wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub ndipo askari
PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi majeruhi
kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi
sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la
mguu wa kushoto.
Amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea
vizuri na katika vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa nusu saa
kabla ya kutulizwa na kikundi cha askari maalumu kilichowahi na
kutuliza vurugu hizo kwa kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa
shwari na hakuna madhara zaidi yaliyojitokeza.
Aidha kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na
tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo
unaendelea na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika
watakaothibitika na ametoa wito kwa waendesha piki piki kuacha
tabia ya kushabikia vurugu ambazo hazina tija na kuwa chanzo cha
kusababisha migogoro isiyokuwa na maana na kusababisha
madhara kwa jamii.
Amewataka waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni
pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa
kupitia viongozi wao ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka
wananchi mkoani Ruvuma kuwa watulivu na kuendelea na shughuli
zao bila hofu yoyote kwani jeshi la polisi liko imara kulinda mali na
maisha yao.
Mwisho.


Wednesday, August 27, 2014

TAMKO LA HISB UT - TAHRIR JUU YA MATESO YA VIONGOZI WA KIISLAM MAHABUSU


“ Nao hawakuona baya lolote kwao ila tu kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa ” (TMQ 85:8)

 Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani kwa nguvu zote mateso, unyama, udhalilishaji na ushenzi mkubwa wanayofanyiwa ndugu zetu Waislamu wakiwemo masheikh, maustadh na wanaharakati wa Kiislamu walioko katika kesi inayodaiwa ya ugaidi, kama walivyoeleza wenyewe karibuni mahkamani jijini Dar es-Salaam na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Sisi katikaHizb tunaweka bayana kwamba: mateso, unyama, ukatili na ushenzi wanaotendewa ndugu zetu Waislamu hao na wengineo ni kwa sababu tu ya Uislamu wao na si vyenginevyo. Kwa sababu kimsingi sheria ya kibaguzi inayoitwa ya ‘ugaidi’ imelazimishwa na
Marekani kwa ajili ya kuwadhulumia Waislamu.  Hizb inauliza kwa kinywa kipana pale viongozi wa kanisa akiwemo Mchungaji Mtikila ambaye mara kwa mara huwekwa korokoroni, kuhojiwa na
Polisi hadi kufungwa jela. Jee kuna siku yoyote aliwahi kufanyiwa ushenzi, mateso na unyama kama wanaofanyiwa ndugu zetu hao Waislamu ?
Tunasema tena, vitendo hivi vya mateso na dhulma ambavyo hufanyiwa Waislamu na vikosi maalumu kwa agizo la Marekani sio mwanzo Tanzania wala sio mwisho. Bali vimeenea duniani kote kuanzia katika kambi za mateso za Marekani za Guntanamo, Balgram, Abu Ghuraib nk.

Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.

Mateso haya hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa, kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu kwa
kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
Pamoja na fedheha hizo za hadharani kutoka kwa taasisi zao wenyewe, bado vikosi hivi vinaonekana kujigubika uziwi na kuendeleza maovu, dhulma, mateso na udhalilishaji wa wazi kwa Waislamu.

Vitendo hivi ni miongoni mwa dalili nyingi za kudhihirisha udhaifu na fedheha kubwa kwa mfumo wa kibepari. Kwanza, kutokuwa na muundombinu thabiti wa ukusanyaji ushahidi, kama kuna ushahidi kamwe katika kesi na badala yake kutegemea utesaji. Pili, dhihirisho la kukosekana uzito shauri/ kesi husika kiasi cha vikosi hivi kumalizia chuki na ghadhabu zao kwa

watuhumiwa kwa kuwatesa. Kwa kuwa wana yakini hakuna kesi itakayoendelea. Tatu, dhana ya kitoto na ndoto za mchana za bwana wao Marekani na mfumo wake wa wa kikafiri wa kibepari kudhani ati kuwatesa Waislamu kutawatisha Umma wa Kiislamu waache na waogope uwajibu wao wa kuhubiri na kutangaza dinibyao ya haki.

Marekani na vikosi vyake vinavyoitwa vya kupambana na ugaidi wanaelea katika ndoto za mchana na kugubikwa na ujinga wa kutojua historia wakidhani kuwa Uislamu utamalizika
kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu. 

Na nne, ni kushindwa watetezi wa mfumo wa kibepari kutetea mfumo wao kwa hoja na dalili. Badala yake katika kutapatapa na khofu ya kumalizika mfumo wao huwa hawana namna ila kutesa Waislamu. Kwa kuwa kimaumbile ubepari
hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za kiakili.

Kimsingi umezaliwa kwa ajili ya kufa! Na punde InshaaAllah utatupwa katika jalala la kihistoria. Kwa kuwa hauna manufaa kwa ubinaadamu zaidi ya madhila na kushindwa juu ya kushindwa.
Umeshindwa ubepari katika siasa ukidai kuna demokrasia kumbe ni nidhamu ya udanganyifu na matajiri. Hudai katiba itokane na watu kumbe tayari wana katiba yao mfukoni, umeshindwa
kiuchumi kwa kuongeza msururu wa makodi na umasikini, huku makampuni ya kibepari yakipora rasilmali kwa baraka za wanasiasa waovu na mikataba ya udanganyifu, umeshindwa katika upande wa kijamii kwa kupitia fikra chafu za
‘uhuru’ (freedoms) kwa kuongeza maovu na mabalaa mbali mbali kwa mwanadamu kuanzia ulevi, zinaa, kupigia debe vitendo viovu vya ushoga, usagaji nk.

Na vitendo hivi vya utesaji na udhalilishaji Waislamu katika mchakato wa kisheria ni kushindwa kuliko dhahiri kukosekana kinachoitwa utawala wa sheria na udhaifu katika taasisi za mahkama za kusimimia haki na sheria. Ajabu na aibu kubwa!
wanashindwa hata kusimamia sheria walizozitunga kwa mikono yao ! Basi nini cha kutarajia kutoka mfumo huu zaidi ya damu na
machozi !
Baada ya yote hayo Hizb inawasisitiza Waislamu kuendelea kuulingania Uislamu wao bila ya khofu wala woga kwa njia ya Mtume SAAW ambayo haihusishi utumiaji wa nguvu wala
mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na
chaguzi zake. Kwa kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala wanaosaidia kudhuru Waislamu.

Aidha, tunawafariji ndugu zetu na Waislamu jumla kwa madhila haya na mengineyo. Lakini pia tunawapa Waislamu bishara ya ushindi wa Umma wetu chini ya kivuli cha dola tukufu ya Kiislamu ya Pili ya Khilafah Rashidah. Dola hiyo haitosahau dhulma hata yenye ukubwa wa punje ya hardali aliyotendewa Muislamu ila itamhukumu dhalimu. Na lau madhaalimu wataondoka duniani kabla ya kurejea dola hiyo. Pia hawatosalimika wala kunusurika na adhabu ya Muumba ambae kamwe hajawasahau, hasahau wala hatosahau na dhulma yao.
 
﴿ ﻭَﻻَ ﺗَﺤْﺴَﺒَﻦَّ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻏَﺎﻓِﻼً ﻋَﻤَّﺎ ﻳَﻌْﻤَﻞُ ﺍﻟﻈَّﺎﻟِﻤُﻮﻥَ ﺇِﻧَّﻤَﺎ ﻳُﺆَﺧِّﺮُﻫُﻢْ ﻟِﻴَﻮْﻡٍ
ﺗَﺸْﺨَﺺُ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻷَﺑْﺼَﺎﺭُ ﴾

“ Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na  yale watendayo madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao .” (TMQ 14: 42
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki

Kumb: 21 / 1435 AH          jumaa, 26th Shawwal 1435 AH
22/08/2014 CE
Tel +255 778 870609
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com
Tovuti  Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info


SIMBA YAICHAPA MAFUNZO

Timu ya Simba ya Dar es salaam leo imeibuka kifua mbele kwa kuifunga timu ya mafunzo mabao mawili kwa bila.
Chini ni picha za mechi hiyo
Wachezaji wa simba wakishangilia Goli la Elias Chaguli aliesajiliwa kutoka ruvu Shooting. Alifunga goli dakika ya 60 ya mchezo huo. Magoli ya Simba yote yamefungwa kipindi cha pili cha mchezo huo wa kirafiki
  
Goli la simba la dakika ya 70 limefungwa na Haruna Chanongo
Watu wakishuhudia mechi hiyo ya kirafiki

kocha wa simba akiongea na waandishi wa habari



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU