Thursday, August 28, 2014
ASKARI WAWILI MBARONI KWA KUJERUHI
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela |
--------------------------------------------------
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili
kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki
aliyejulikana kwa jina la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma
mjini Songea.
Akizungumza kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo
Msekhela amesema tukio hilo limetokea Agosti 26 mwaka huu
majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea
ambapo askari polisi wawili PC Waziri mwenye namba G 5075 na
PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria na piki piki ya
polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina ya Yamaha CC 250
katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki huyo
kwa kumpiga risasi.
Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi
na askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo
iliyokuwa imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye
alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na
mwendesha piki piki aliyejulikans kwa jina moja la Agrey ambaye
alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa piki piki iliyokamatwa na askari
hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.
Ameitaja piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni
aina ya San Lug yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada
ya mwendesha piki piki huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini
wake Agrey alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa
waendesha piki piki maarufu kama Yebo yebo ambao walianza
kuwarushia mawe askari hao huku majeruhi akiwa ameshika mtutu
wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub ndipo askari
PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi majeruhi
kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi
sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la
mguu wa kushoto.
Amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea
vizuri na katika vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa nusu saa
kabla ya kutulizwa na kikundi cha askari maalumu kilichowahi na
kutuliza vurugu hizo kwa kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa
shwari na hakuna madhara zaidi yaliyojitokeza.
Aidha kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na
tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo
unaendelea na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika
watakaothibitika na ametoa wito kwa waendesha piki piki kuacha
tabia ya kushabikia vurugu ambazo hazina tija na kuwa chanzo cha
kusababisha migogoro isiyokuwa na maana na kusababisha
madhara kwa jamii.
Amewataka waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni
pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa
kupitia viongozi wao ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka
wananchi mkoani Ruvuma kuwa watulivu na kuendelea na shughuli
zao bila hofu yoyote kwani jeshi la polisi liko imara kulinda mali na
maisha yao.
Mwisho.
Wednesday, August 27, 2014
TAMKO LA HISB UT - TAHRIR JUU YA MATESO YA VIONGOZI WA KIISLAM MAHABUSU
“ Nao hawakuona baya lolote kwao ila tu kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa ” (TMQ 85:8)
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani kwa nguvu zote mateso, unyama, udhalilishaji na ushenzi mkubwa wanayofanyiwa ndugu zetu Waislamu wakiwemo masheikh, maustadh na wanaharakati wa Kiislamu walioko katika kesi inayodaiwa ya ugaidi, kama walivyoeleza wenyewe karibuni mahkamani jijini Dar es-Salaam na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Sisi katikaHizb tunaweka bayana kwamba: mateso, unyama, ukatili na ushenzi wanaotendewa ndugu zetu Waislamu hao na wengineo ni kwa sababu tu ya Uislamu wao na si vyenginevyo. Kwa sababu kimsingi sheria ya kibaguzi inayoitwa ya ‘ugaidi’ imelazimishwa na
Marekani kwa ajili ya kuwadhulumia Waislamu. Hizb inauliza kwa kinywa kipana pale viongozi wa kanisa akiwemo Mchungaji Mtikila ambaye mara kwa mara huwekwa korokoroni, kuhojiwa na
Polisi hadi kufungwa jela. Jee kuna siku yoyote aliwahi kufanyiwa ushenzi, mateso na unyama kama wanaofanyiwa ndugu zetu hao Waislamu ?
Tunasema tena, vitendo hivi vya mateso na dhulma ambavyo hufanyiwa Waislamu na vikosi maalumu kwa agizo la Marekani sio mwanzo Tanzania wala sio mwisho. Bali vimeenea duniani kote kuanzia katika kambi za mateso za Marekani za Guntanamo, Balgram, Abu Ghuraib nk.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Mateso haya hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa, kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu kwa
kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Mateso haya hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa, kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu kwa
kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
Pamoja na fedheha hizo za hadharani kutoka kwa taasisi zao wenyewe, bado vikosi hivi vinaonekana kujigubika uziwi na kuendeleza maovu, dhulma, mateso na udhalilishaji wa wazi kwa Waislamu.
Vitendo hivi ni miongoni mwa dalili nyingi za kudhihirisha udhaifu na fedheha kubwa kwa mfumo wa kibepari. Kwanza, kutokuwa na muundombinu thabiti wa ukusanyaji ushahidi, kama kuna ushahidi kamwe katika kesi na badala yake kutegemea utesaji. Pili, dhihirisho la kukosekana uzito shauri/ kesi husika kiasi cha vikosi hivi kumalizia chuki na ghadhabu zao kwa
watuhumiwa kwa kuwatesa. Kwa kuwa wana yakini hakuna kesi itakayoendelea. Tatu, dhana ya kitoto na ndoto za mchana za bwana wao Marekani na mfumo wake wa wa kikafiri wa kibepari kudhani ati kuwatesa Waislamu kutawatisha Umma wa Kiislamu waache na waogope uwajibu wao wa kuhubiri na kutangaza dinibyao ya haki.
Marekani na vikosi vyake vinavyoitwa vya kupambana na ugaidi wanaelea katika ndoto za mchana na kugubikwa na ujinga wa kutojua historia wakidhani kuwa Uislamu utamalizika
kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu.
kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu.
Na nne, ni kushindwa watetezi wa mfumo wa kibepari kutetea mfumo wao kwa hoja na dalili. Badala yake katika kutapatapa na khofu ya kumalizika mfumo wao huwa hawana namna ila kutesa Waislamu. Kwa kuwa kimaumbile ubepari
hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za kiakili.
hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za kiakili.
Kimsingi umezaliwa kwa ajili ya kufa! Na punde InshaaAllah utatupwa katika jalala la kihistoria. Kwa kuwa hauna manufaa kwa ubinaadamu zaidi ya madhila na kushindwa juu ya kushindwa.
Umeshindwa ubepari katika siasa ukidai kuna demokrasia kumbe ni nidhamu ya udanganyifu na matajiri. Hudai katiba itokane na watu kumbe tayari wana katiba yao mfukoni, umeshindwa
kiuchumi kwa kuongeza msururu wa makodi na umasikini, huku makampuni ya kibepari yakipora rasilmali kwa baraka za wanasiasa waovu na mikataba ya udanganyifu, umeshindwa katika upande wa kijamii kwa kupitia fikra chafu za
‘uhuru’ (freedoms) kwa kuongeza maovu na mabalaa mbali mbali kwa mwanadamu kuanzia ulevi, zinaa, kupigia debe vitendo viovu vya ushoga, usagaji nk.
Na vitendo hivi vya utesaji na udhalilishaji Waislamu katika mchakato wa kisheria ni kushindwa kuliko dhahiri kukosekana kinachoitwa utawala wa sheria na udhaifu katika taasisi za mahkama za kusimimia haki na sheria. Ajabu na aibu kubwa!
wanashindwa hata kusimamia sheria walizozitunga kwa mikono yao ! Basi nini cha kutarajia kutoka mfumo huu zaidi ya damu na
machozi !
Baada ya yote hayo Hizb inawasisitiza Waislamu kuendelea kuulingania Uislamu wao bila ya khofu wala woga kwa njia ya Mtume SAAW ambayo haihusishi utumiaji wa nguvu wala
mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na
chaguzi zake. Kwa kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala wanaosaidia kudhuru Waislamu.
mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na
chaguzi zake. Kwa kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala wanaosaidia kudhuru Waislamu.
Aidha, tunawafariji ndugu zetu na Waislamu jumla kwa madhila haya na mengineyo. Lakini pia tunawapa Waislamu bishara ya ushindi wa Umma wetu chini ya kivuli cha dola tukufu ya Kiislamu ya Pili ya Khilafah Rashidah. Dola hiyo haitosahau dhulma hata yenye ukubwa wa punje ya hardali aliyotendewa Muislamu ila itamhukumu dhalimu. Na lau madhaalimu wataondoka duniani kabla ya kurejea dola hiyo. Pia hawatosalimika wala kunusurika na adhabu ya Muumba ambae kamwe hajawasahau, hasahau wala hatosahau na dhulma yao.
﴿ ﻭَﻻَ ﺗَﺤْﺴَﺒَﻦَّ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻏَﺎﻓِﻼً ﻋَﻤَّﺎ ﻳَﻌْﻤَﻞُ ﺍﻟﻈَّﺎﻟِﻤُﻮﻥَ ﺇِﻧَّﻤَﺎ ﻳُﺆَﺧِّﺮُﻫُﻢْ ﻟِﻴَﻮْﻡٍ
ﺗَﺸْﺨَﺺُ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻷَﺑْﺼَﺎﺭُ ﴾
“ Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na yale watendayo madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao .” (TMQ 14: 42
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Kumb: 21 / 1435 AH jumaa, 26th Shawwal 1435 AH
22/08/2014 CE
Tel +255 778 870609
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com
Tovuti Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Kumb: 21 / 1435 AH jumaa, 26th Shawwal 1435 AH
22/08/2014 CE
Tel +255 778 870609
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com
Tovuti Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info
SIMBA YAICHAPA MAFUNZO
Timu ya Simba ya Dar es salaam leo imeibuka kifua mbele kwa kuifunga timu ya mafunzo mabao mawili kwa bila.
Chini ni picha za mechi hiyo
Chini ni picha za mechi hiyo
![]() |
Goli la simba la dakika ya 70 limefungwa na Haruna Chanongo |
![]() |
Watu wakishuhudia mechi hiyo ya kirafiki |
![]() |
kocha wa simba akiongea na waandishi wa habari |
YANGA YAIFUNIKA SIMBA ZANZIBAR
Katika mechi hizo zilizofanyika jumapili jioni na usiku Yanga iliteremka dimbani kupambana na Shangani fc inayoshiriki daraja la pili wilaya ya mjini hapa unguja na Simba ikapambana na Kilimani City nayo pia inashiriki katika daraja hilo hilo la pili wilya ya mjini, katika pambano la kwanza la Yanga liliofanyika majira ya saa 10 jioni liliingiza shilingi mil 7.3, wakati lile la pili liloanza majira ya saa 2 usiku lilioihusisha timu ya Simba liliingiza shilingi mil 3.1 tu na kuzusha maswali mengi sana kwa wadau.
kwa kuwa pambano hilo lililofanyika usiku na kuhudhuriwa na watu wengi sana kuliko wale wa mchana,hali hiyo ilifanya viongozi wa Simba wa mjini hapa wakiongozwa na Bw. Abdul Mshangama kuhoji kulikoni wao wapate mapato kiduchu namna hiyo na wakati kwenye mechi yao ndiyo kulikuwa na watu wengi na wamewatupia lawama kuwa Kilimani City wamechakachua mapato hayo.
Viongozi wa Mlimani walipatwa na kigugumizi na kuonyesha kusikistishwa na hilo licha ya viongozi hao kuomba radhi. Hali iliyosababisha hasira za viongozi wa Simba na kuwaambia wao walikuwa wamejenga urafiki lakini wameonyesha si waminifu katika pesa hizo ndogo
"hizo pesa ni ndogo na kusema kuwa kama wao Kilimani ndiyo waliomba na kuna makubaliano walikubaliana juu ya usimamizi na mgawanyo wa mechi mapato hayo na hata kama watataka waje Dar tutacheza nao na hata kama wanahitaji msaada wa kipesa tutawapa bila shida ila hawakutufurahisha kwa kweli" alisema kiongozi mmoja wa simba
Nayo ZFA wilaya ya mjini kupitia katibu wake Yahya Juma Ally wameshngazwa na tukio hilo huku wakiwatupia lawama viongozi hao wa Kilimani
"kwa kuwa waliwaambia viongozi wa Kilimani City walete vitabu vyote vya tiketi ili vigongwe muhuri wa ZFA na baadae sisi tuje kusimamia hata milangoni lakini wenzetu walienda kinyume wakaleta vitabu kidogo tu na hata milangoni wakawa wao wenyewe bila kuishirikisha ZFA" alisema kiongozi wa ZFA
Kwa hili lililotokea ZFA wilaya mjini tumesikitishwa sana na fedheha hii tuliyopewa na timu ya kilimani City na tutajitahidi lisitokee tena kwenye mechi zijazo aliongeza kiongozi huyo wa ZFA.
Tuesday, August 26, 2014
WAKONGWE WA REAL MADRID WAKIELEKEA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro.
Subscribe to:
Posts (Atom)