Facebook Comments Box

Thursday, April 10, 2014

HABARI YA KIUNGO WA ARSENAL ALIE JIUNGA NA JIHAD


Kiungo wa zamani wa Arsenal na Real Madrid
anayekipiga katika klabu ya Lokomotiv Moscow
Lassana Diarra amekanusha madai kwamba ni
mfuasi wa vita ya kidini nchini Syria.
Wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Diarra (29)
alijiunga na vita inayoendelea Syria baada ya
kutolewa kwa video inayomuonyesha mtu akiwa
kajifunika uso huku akijitambulisha kwamba ni
Lassana Diarra.
Hata hivyo kiungo huyu wa timu ya taifa ya
Ufaransa ambae aliwahi pia kuitumikia
Portsmouth na Chelsea, ametoa taarifa rasmi
kupitia wakili wake na kusema hahusiki kabisa
na hiyo video.
“Hajawahi kukanyaga nchini Syria, yeye ni mwanasoka
anayeichezea Lokomotiv Moscow,” amesema
Mwanasheria wake.


WATOTO WA TANZANIA WALIOSHINDA KOMBE LA DUNIA WAWASILI NCHINI

''Tunaipongeza timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kuchukua ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani majuzi (Aprili 6
mwaka huu) baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali
uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Ushindi kwa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa
kituo cha Mwanza ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na
wadhamini na wafadhili walioiwezesha kushiriki fainali hizo kwa
mara ya pili mfululizo.
Vilevile ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa
mpira wa miguu kuwa watoto wa mitaani ni sehemu tu ya vipaji
vilivyotapaa nchini, hivyo iliyopo ni kuvisaka na kuvibaini vipaji
hivyo kwa ajili ya ustawi wa mchezo huo nchini.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tutaendelea
kushirikiana na kituo hicho cha Mwanza, na vingine vyote ambavyo
vinajishughulisha na mchezo huu, lengo likiwa ni kuundeleza na
hata kutoa ajira kwa vijana hapo baadaye kupitia mpira wa miguu.
Timu hiyo imerejea nchini leo ambapo imetua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 na nusu jioni kwa ndege
ya Emirates''
Viongozi wa watoto wa mitaani wakiwasili na vikombe walivyo nyakua huko Brazili 


Wednesday, April 9, 2014

RAIS KIKWETE ACHAGULIWA KIONGOZI BORA BARANI AFRIKA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango
Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la
kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima
hiyo itatolewa jioni ya leo, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe
iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa
ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao
hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa
watu wao na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake
usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya
utawala bora.

CHANZO: EAST AFRICA RADIO


Saturday, March 15, 2014

HUU NDIO MFANO WA KUIGWA ULIO ONESHWA NA VIONGOZI WA YANGA

Uongozi wa klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans umeonyesha mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa soka nchini siku moja baada ya kurudi kutoka Misri walipoenda na timu kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya  klabu hiyo ni kwamba viongozi wa msafara wa Yanga chini ya mkuu wa msafara huyo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga umerudisha kiasi cha millioni 39 klabuni kutoka kwenye fedha walizopewa kwa ajili ya matumizi kwenye safari yao nchini Misri.

"Eeh bwana safari hii kweli tuna viongozi wenye nia ya dhati ya kuiongoza vizuri Yanga, Sanga na viongozi wenzie walioenda Misri walipewa fungu la bajeti kwa ajili ya matumizi yote ya klabu nchini Misri, lile fungu lilikuwa litumike lote, lakini tofauti na viongozi wote wa misafara waliopita, Sanga na wenzake wameweza kurudisha millioni 39 kutoka katika fedha walizopewa. Haijawahi kutokea kwenye klabu hii kwa kweli, huko nyuma kitendo kama hichi hakikuwahi kutokea, hapa klabuni kila aliyesikia kuhusu hilo jambo ameshutushwa.
"Zile fedha zilikuwa tayari zimeshatolewa kwa matumizi hivyo hata kama wangeamua kuzila hakuna ambaye angeulizia, hawa jamaa ni waadilifu na wana mapenzi ya kweli na klabu," kilisema chanzo hicho cha habari.


Saturday, March 1, 2014

PICHA: YANGA ILIPO INYONYOA AL AHLY

Young African Sports Club leo imefanya yale ambayo watanzania wengi walio tarajia baada ya kuinyonyoa Al ahly kwa bao moja kwa bila.
Bao lilifungwa na Nadir Haroub katika dakika ya 82.
Yanga ndio iliocheza mpira safi na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
Washabiki wengi wanasema kwa mpira walio onesha Yanga waarabu watatolewa na Yanga.

Tunawatakia Yanga kila la heri.
Chini ni picha za mpambano huo zikiwemo za washabiki wa Simba ambao waliamua kung'oa viti na kuwarushia washabiki wa Yanga.



Thursday, February 13, 2014

OKWI RUKSA KUCHEZA YANGA

Taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema FIFA imebaliki taratibu za uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka SC Villa kujiunga na Yanga.
Taarifa kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF zinasema FIFA imemruhusu mchezaji huyo kuendelea kucheza, nakuhusu suala la deni la Simba shirikisho hilo limesema bado linalifanyia kazi.


Sunday, February 9, 2014

DAR YOUNG AFRICANS YAWACHAPA VIBONDE KOMOROZINE BAO 7 KWA 0

Hamis Kiiza hapa anaonekana akifunga bao la nne katika saba walizoshinda hapo jana.

Picha zaidi zitakujia baadae.



KIPIGO CHA BAO 5 KWA 1 ILICHOPATA ARSENAL CHAMCHANGANYA WENGER ADONDOKA CHINI

Timu ya Arsenal ilipata kipigo cha bao 5 kwa moja kutoka kwa Liverpool ndani ya Anfield jana Jumamosi baada ya timu hizo kukutana katika ligi kuu ya England. 

Wenyeji walikuwa wa kwanza kujipatia bao la kuongoza katika dakika ya kwanza tu ya mchezo huo kupitia kwa Beki wake SKRTEL ambaye aliifungia tena timu yake dakika ya 10 ya mchezo. Wafungaji wa mabao mengine ni STERLING dakika ya 15 na 52, STURRIDGE dakika ya 20.

Chelsea nao waliwachapa Newcasle bao 3 kwa 0, wakati Man City wakilazimishwa sare ya 0-0 na Norwich na kufanya Msimamo wa ligi hiyo kubadilika na kuwa Chelsea nafasi ya Kwanza, Arsenal ni yapili, Man City ya tatu na Liverpool imebaki katika nafasi yake ya nne pamoja na ushindi wake huo mnono.




Thursday, January 16, 2014

MELI YA TITANIC YAANZA KUTENGENEZWA UPYA

china-titanic-replica-6d-tragedy-simulator-1-690x494
Na Mwandishi Wetu, 
WENGI wa watu nchini China wanapendelea ujenzi wa majengo makubwa ya kihistoria na magari kadhaa yenye muonekano wa alama ya uchina kama ishara ya kuonyesha ufanisi wao katika uvumbuzi wa vitu mbalimbali duniani.
Lakini basi tena, wachina ni watu katika jamii wanaopenda kufanya mambo makubwa na tofauti na ni wazalishaji wa vitu vingi vya hapa leo duniani, sasa wachina wanatengeneza meli kubwa kwa mfano wa meli maarufu ya Titanic.
Meli ya Titanic iliyozama mwaka 1914 karibu karne moja iliyopita na kuua watu karibu elfu moja, sasa kampuni kutoka uchina ya Star Investment Group katika mkoa wa Sichuan itatumia dola za kimarekani 165 milioni katika kujenga upya meli mfano wa Titanic.

china-titanic-replica-6d-tragedy-simulator-3
Meli hiyo mpya ya wachina itafanana kabisa na meli ya Titanic iliyozama vibaya kwenye kina cha bahari karne moja iliyopita. Meli hiyo itajengwa kwa ushirikiano na kampuni ya serikali ya China Ship building Corporation ya Wuchang inatumika kama sehemu ya hifadhi ya makumbusho katika mkoa wa Sichuan.
Katika meli hii ya replica ni ishara ya uvumbuzi uliotukuka kutoka kwa wachina na watazamiwa kuingiza mamilioni ya fedha kama riba kutokana na alama ya Titanic duniani.


VIDEO: TEMA MATE TUWACHAPE - MADEE









 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU