Facebook Comments Box

Thursday, September 5, 2013

VIDEO: VURUGU ZA BUNGENI LEO




PICHA: ANGALIA PICHA ZA VURUGU BUNGENI LEO HII





Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.

****
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.

Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.

Mara baada ya  zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.


PICHA: RAIS KIKWETE ALIPO KUTANA NA RAIS KAGAME







WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUSOTA NA FOLENI ZA BARABARANI


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wataendelea kukumbwa na kero ya msongamano wa magari barabarani baada ya mpango wa serikali wa kupunguza tatizo hilo kupitia ujenzi wa barabara zilizopo nje ya jiji kukwama kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo wakandarasi wanaojitokeza kuomba kujenga kuomba  kiasi kikubwa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale, alisema mpango huo wa kujenga barabara za nje ya jiji upo ingawa unakabiliwa na changamaoto mbalimbali zikiwamo watu kutojitokeza kuomba kazi ya kujenga na wanaojitokeza kuomba kiasi kikubwa cha fedha hatua iliyoifanya serikali kurudia kutangaza tenda.

Katika mkutano wa Bunge la bajeti mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alitangaza kwamba kwa  mwaka 2013/2014 serikali itajenga barabara za nje ya jiji la Dar es Salaam ili kukabiliana na msongamano wa magari.

Alizitaja kuwa ni pamoja na inayoanzia Mbezi Beach Tangi Bovu hadi Mbezi Shamba kupitia Goba, Mbezi Shamba hadi Tegeta kupitia Goba na ile ya Mbezi Shamba hadi Uwanja wa Ndege kupitia Kinyerezi.

Ahadi nyingine aliyotoa Dk. Magufuli kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014 ni ujenzi wa barabara za juu katika maeneo ya Tazara, Mwenge na Ubungo mipango ambayo mpaka sasa haijaanza kutekelezwa.

Wakati ahadi hizo zikichelewa kuanza, Tanroads  imesema barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha Lami na nyingine Changarawe kulingana na upatikanaji wa fedha.

Kuhusu bomoa bomoa mbalimbali zinazoendelea jijini Dar es Salaam, Mfugale alisema baadhi hawahusiki nazo na kutoa mfano nyumba zilizomolewa wiki iliyopita eneo la Mbezi Beach.

Alisema wananchi wakiona Tingatinga linabomoa mahali popote wanajua ni Tanroads na kusema kuwa baadhi ya maeneo yanabomolewa kwa ajili ya kupitisha bomba la maji au shughuli zingine za serikali siyo lazima iwe ujenzi wa barabara.

SOURCE: NIPASHE


WAZEE YANGA WAMKATAA KATIBU NA MHASIBU MHINDI

akilimalii_6c882.jpg
WAZEE wa Yanga waliokasirika na 'kuipiga laana' timu baada ya kutofautiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu wakati huo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga ikapigwa 5-0 na Simba SC mwaka juzi, wameingia katika mgogoro mwingine na uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji.
 
Wazee hao chini ya kinara wao, Ibrahim Ally Akilimali wanaingia katika mtafaruku na uongozi wa Manji, kiasi cha mwezi mmoja na ushei kabla ya mchezo mwingine dhidi ya watani wa jadi, Simba SC Oktoba 20, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Hatumtaki huyo Mkenya; Kutoka kulia Mzee Bilal Chakupewa, Ibrahim Akilimali na Hashim Muhika. Wazee hao wamesema hawatambui ajira ya Mkenya.
 
Katika Mkutano wao na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Wazee hao wanapinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya kutoka Kenya.
 
Katibu Mkuu mpya wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.
 
Akizungumza na Waandishi wa jhabari klabu leo, Mwenyekiti wa Wazee hao, Ibrahim Akilimali amesema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, lazima awe mwanachama wa klabu hiyo, hivyo walivyofanya uongozi ni kinyume kabisa na Katiba inavyotaka.
 
"Mpaka sasa sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama wa klabu hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na kumpa ushirikiano.
"Kazi za Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu, hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu, tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi," alisema Akilimali
 
Alisema wao wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.
Akilimali alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.
 
Alimfananisha Mkenya huyo ni mtu aliyeingia kwa njia za panya katika klabu hiyo, kwa kuwa hawana mwanachama wa aina yake kwenye leja ya wanachama wa Yanga.
Alisema wamekuwa na kawaida ya kupewa taarifa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Manji kama kunakuwa na jambo lolote ambalo wamepanga kulifanya kwa maslahi ya Yanga, lakini hawakuambiwa kuhusu ajira ya Mkenya huyo.
 
"Huyu mtu tunamwona ni 'kanjanja' aondoke haraka sana, sisi wana Yanga hatumuitaji kabisa," alisema Akilimali.
 
Wakati huo huo, mwanachama wa klabu hiyo, Said Motisha alisema Yanga itagawanyika kwa hilo, kwani hawatakubali wazawa kunyimwa ajira wakati wanasifa ya kufanya kazi.


Tuesday, September 3, 2013

KING CRAZY GK ARUDI KWENYE GAME NA HII NDIO VIDEO YAKE MPYA




PACHA WA ALIEFANYIWA UPASUAJI KWA MASAA NANE ATOLEWA CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI MUHIMBILI

pacha1 2e1b7
Mtoto Kudra aliyekuwa ameunganika na kiwiliwili cha pacha mwenza, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mtoto huyo alifanyiwa upasuaji Alhamisi iliyopita katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na kulazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), lakini mwishoni mwa wiki iliyopita alitolewa katika wodi hiyo.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Pili Hija, alisema hivi sasa Kudra ananyonya vizuri na kwamba amekuwa akitaka kufanya hivyo kila wakati .
"Kwa kweli kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zimemweka hai mpaka leo hii, nilikuwa nimeshakata tamaa kuwa nampoteza mwanangu, nazidi kumuomba Mungu amwekee mkono wake apone kabisa," alisema Hija.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Dk Zaitun Bokhary, alisema mtoto huyo anaendelea vizuri na mwishoni mwa mwezi huu atafanyiwa upasuaji mwingine.
"Tunamwacha achangamke kwanza, mwishoni mwa mwezi huu tutamfanyia upasuaji mwingine wa kumwekea njia ya muda ya kutolewa haja kubwa, kwa kumpasua ubavuni baada ya hapo ataruhusiwa kwenda nyumbani," alisema Dk Bokhary.
Kudra alipewa jina hilo Alhamisi usiku, saa kadhaa baada ya upasuaji kufanyika chini ya jopo la madaktari saba, walioongozwa na Dk Hamis Shaaban, mtaalamu wa Ubongo na Uti wa Mgongo kutoka Moi.
Alizaliwa Agosti 18, baada ya mwanamke huyo kujifungulia nyumbani watoto pacha, huku mmoja akiwa hajakamilika viungo vyote. Pia, kiwiliwili kilichoungana hakikuwa na kichwa, macho, maini, figo ila alikuwa na mshipa mmoja wa fahamu ambao ulikuwa umeshikana na mwenzake na kulazimisha madaktari hao kumfanyia upasuaji.
 
CHANZO:MWANANCHI


TUHUMA, KASHFA NA UFISADI MALIASILI

Imeandikwa na Danson Kaijage, Dodoma, Tanzania Daima — 
 
WAKATI mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, akimtuhumu Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kuibeba kampuni ya uwindaji ya Leopard Tours Ltd, mwenyewe amejibu mapigo akidai mbunge huyo hajafanya utafiti.

Msigwa aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuwa Kagasheki alitumia nafasi yake kuiarifu kampuni hiyo kuipatia ekari tano kwa gharama ya dola za Kimarekani 30,000 nusu ya gharama za kawaida dola 60,000 kwa ekari kumi.

Mbunge huyo ambaye pia ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa wizara hiyo, alisema kuwa Kagasheki anaendesha wizara kwa kukiuka sheria na taratibu akitumia mamlaka vibaya.

Msigwa alisema kuwa Kagasheki tangu alipoingia madarakani na kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), sasa hifadhi inaendeshwa bila bodi jambo ambalo ni kinyume.

Alidai kuwa waziri huyo alifanya maamuzi hayo ya kuibeba kampuni hiyo ya uwindaji bila kuzingatia sheria na kanuni za ugawaji wa vitalu na kwamba alivunja sheria kwa kufanya uamuzi wa moja kwa moja na Leopard Tours wa kushusha viwango vilivyowekwa kisheria bila kutoa tangazo la serikali.

Msigwa pia aliibua tuhuma nyingine akidai kuwa Kagasheki ama kwa makusudi au kutokujua kuwa ana
maslahi binafsi ya mahusiano na mbunge wa viti Maalumu wa Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (CCM), na kumkingia kifua ili taasisi yake ya Catherine Foundation ipate msaada wa sh milioni 10 kutoka NCAA.

“Msaada huo si tu ulikiuka kanuni za msaada ambao unaelekezwa katika shughuli za msaada wa kijamii kupewa kiasi kisichozidi sh milioni 2 lakini mradi huo wa Catherine ulipewa fedha hizo huku dokezo la maombi ya msaada huo likionyesha watendaji wa NCAA wakilalamika. Walitoa mapendekezo mara mbili, kwanza kwa kupitia meneja wa maendeleo ya jamii kuwa hakuna bajeti ya kusaidia msaada huo kutoka idara ya maendeleo ya jamii labda wafikiriwe kupitia fungu la donesheni,” alieleza Msigwa.

Aliongeza kuwa nyaraka zinaonyesha kwamba kaimu mhifadhi wa Ngorongoro, alimjibu meneja maendeleo ya jamii kuwa fungu la donesheni halina fedha za kutosha, hivyo ni bora Magige ajibiwe na asubiri mpaka mwaka wa fedha ujao.

Msigwa alifafanua kuwa dokezo hilo lilisainiwa Desemba 14 mwaka jana: “Jambo la kushangaza na kutia walakini ni kuwa kaimu mhifadhi kwa shinikizo alimuelekeza mhasibu kuilipa Catherine Foundation kiasi cha milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 18 Juni, mwaka huu, ukiwa ni mwaka wa fedha wa 2012/13 kinyume na mapendekezo yake ya awali.”

Alisema kuwa wanataka kujua kaimu mhifadhi alitumia kigezo gani kuilipa taasisi hiyo fedha hizo za msaada wa ununuzi wa madawati tofauti na kiwango kilichowekwa cha sh milioni 2.

Kagasheki ajibu

Akijibu tuhuma hizo, Kagasheki alisema kuwa anamfahamu Msigwa kwa vile hiyo si mara yake ya kwanza kutoa tuhuma za uongo dhidi yake: “Msigwa alishawahi kusema nijiuzulu kwamba nimeshindwa kushughulikia ujangili kwa kuwa eti nashughulika na watu wadogo (dagaa) na kuwaacha mapapa (viongozi),” alisema.

Kagasheki alifafanua kuwa tatizo analoliona kwa Msigwa ni kukurupuka bila kufanya utafiti wa kina na kuanza kutuhumu watu kwa sababu binafsi anazozijua yeye: “Msigwa ana chuki na mimi na hii ilitokana na yeye kuondolewa kwenye Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira; anadhani nilishawishi aondolewe kumbe yalikuwa matakwa ya Spika,” alisema.

Alisisitiza kuwa kwa vile Msigwa amejitokeza kuisemea Ngorongoro ni dhahiri sasa anaamini tetesi zilizopo dhidi yake kuwa anatumika kuwatetea vigogo walioondolewa kwa tuhuma za ufisadi: “Ngorongoro kuna ufisadi wa kutisha, subirini kidogo ripoti yake inakamilika mtajionea hao watu anaowatetea walifanya nini huko,” alisema.

Kuhusu madai ya kuibeba kampuni ya uwindaji, Kagasheki alisema kuwa mwindaji huyo amekuwa nchini akifanya kazi zake kihalali na kutoa ajira kwa wazawa na kwamba uamuzi wake ulikuwa wa busara kwani NCAA walitaka kumchakachua: “Huyu aliomba eneo kujenga kambi lakini lililopatikana halikufikia hata nusu sasa wakawa wanataka kumuuzia kila kilomita kwa dola 60,000 ndipo nikaagiza auziwe kwa nusu yake. Hapa nilifanya kosa gani wakati nilidhibiti ufisadi?” alihoji.

Alisisitiza kuwa tayari anazo taarifa za Msigwa kutumiwa na kundi linalompiga vita ndani ya wizara hiyo na kaapa kwamba kamwe hawatashinda.

Kuhudu madai ya kuishinikiza NCAA kumpa msaada Magige, waziri huyo alisema maneno hayo ni ya kitoto zaidi kwani kama angetumia wadhifa wake kumkingia kifua asingepewa fedha kidogo kiasi hicho: “Ni kweli Magige ana taasisi yake na wamekuwa wakiomba fedha maeneo mengi kusadia yatima na wahitaji wengine lakini sina taarifa kama hata aliomba fedha NCAA; Msigwa ana ajenda yake,” alisema.

Magige awaka

Akizungumzia tuhuma hizo, Magige alisema taasisi hiyo ni kama zingine na hivyo kumshangaa Msigwa kuihusisha na mahusiano binafsi ya watu.

Alikiri kuomba msaada NCAA na kupewa kiasi hicho cha sh milioni 10 lakini akasema huo ni uamuzi wao kwani hawakuwapangia kiwango.

“Tuliandika barua ya maombi tukapeleka; ikakaa muda mrefu lakini baadaye wakatuita na kutupa msaada huo. Mimi nadhani kungelikuwa na shinikizo la waziri ningepewa fedha nyingi zaidi ya hizo! Msigwa ni mchungaji, sisi tunapaswa kujifunza ukweli kutoka kwake sasa iweje anasingizia watu na kuwazulia mambo ya uongo jamani? Amekumbwa na nini?” alihoji Magige.

Source: wavuti



ANGALIA VIDEO YA KIBAO KIPYA CHA DIAMOMD PLATNUMZ - MY NUMBER ONE KATIKA HD




FELLAINI ATAMBULISHWA MANCHESTER UNITED

Fellaini athibitishwa kwenda Manchester United kwa £27.5



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU