
Thursday, June 6, 2013
MAREKANI WAANDAA SHERIA ITAKAYO KATAZA WATU KUVAA MLEGEZO

Sina
shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye
majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina
lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama
ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao
hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa
style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo
ambao bado wako shuleni.
Katika hali
ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa
Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza
kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza
mitaani.

Sheria
hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na
sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa
Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa
amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio
nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
HII NDIO KAULI YA M 2 THE P BAADA YA KUFIKA TANZANIA KUMZIKA MANGWEA

Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini
Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani
Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya
leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2
The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa
nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake
Mangwea. “Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P
nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili
Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi
changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea
asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi,
asanteni,” alisema. Msikilize hapa
PICHA ZA UTOAJI WA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU MANGWEA MOROGORO
Meza kuu
hii ikiwa ni maandalia ya kuuwaga mwili wa msanii marehemu Albert
Mangwea aliyefariki dunia na anatarajiwa kuzikwa leo mkoani
morogoro.Utaratibu huu umeandaliwa katika uwanja wa jamuhuri mkoani
morogoro kwa lengo la kuwapa fursa wakazi wa mji huo kupata nafasi za
kuuwaga mwili huo kabla ya maziko
Umati
mkubwa wa wakazi wa morogoro waliojitokeza katika zozi za kuwaga mwili
wa msanii huyo mchana huu kabla ya maziko yake leo.Marehemu albert mangwea alifariki wiki
iliyopita nchini afrika kusini na maziko yake yatafanyika leo mkoani
hapa.

Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.

Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera asubuhi hii amefika nyumbani kwa Mama
Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi
wote wa mkoa wa Morogoro. Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza
umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za
kuaga mwili wa Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini
Afrika Kusini. Mangwea anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda
nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake
mzazi Mzee Keneth Mangwea.
MAJANGA YAZIDI MUANDAMA MR. NICE SASA MKATABA WAKE NA GRAND PA RECORDS YA KENYA WAVUNJWA
Mwanamuziki aliyevumbua staili ya muziki ya TAKEU (Tanzania Kenya Uganda), Mtanzania Lukas Mkenda aka Mr Nice amepoteza mkataba wake na kampuni ya kurekodi muziki ya nchini Kenya, kwa kile kilichoelezwa na kampuni hiyo kuwa ni tabia ya Mr Nice ya uvivu, ulevi, asiyeaminika na asiye na ushirikiano.
Zaidi ya maandishi yaliyoandikwa na GrandPa Records kwenye ukurasa wao wa Facebook, pia wamezungumzia suala hilo walipohojiwa na kituo cha EA Radio ambapo wamesema Mr Nice amesema ataendelea kubaki mjini Nairobi nchini Kenya akitafuta kujiweka sawa.
Wednesday, June 5, 2013
KOCHA WA YANGA AWASILI KWA AJILI YA KUINOA TIMU KWA AJILI YA MSIMU MPYA
![]() |
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Ernie
Brandts (kulia) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar
es Salaam usiku wa leo akitokea kwao Uholanzi kwa mapumziko mafupi
baada ya kumaliza msimu, tayari kuanza maandalizi ya kikosi chake kwa
msimu mpya. Aliyemlaki kushoto ni Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh.
|
![]() |
Anaondoka Airport |
![]() |
Baada ya kutua, kitu cha kwanza aliwasha simu yake |
![]() |
Anafungua mlango wa gari lake apakie mizigo |
![]() |
Anafungua mlango wa nyuma apakie mizigo |
![]() |
Hahitaji msaada wa mtu, anapakia mwenyewe |
![]() |
Anafunga mlango baada ya kupakia |
![]() |
BIN ZUBEIRY anaondoka baada ya kumaliza kazi yake |
![]() |
Brandts naye anapanda gari lake |
![]() |
Anapiga stata... |
![]() |
Anaondoka Airport |
POLISI WATUMIA MBWA KUTAWANYA WATU LEADERS BAADA MUDA WA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KUISHA

ASKARI wa Jeshi la Polisi walilazimika kutumia Mbwa kuwatawanya mamia ya Watanzania waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea lakini wakashindwa baada zoezi hilo kukatishwa.
Mangewa alifariki Dunia nchini Afrika Kusini katika Jiji la Johannesburg Mei 28 mwaka huu na kusafirishwa kuja nchini jana jioni, mamia hao wa watanzania wameshindwa kuuaga mwili wa kipenzi chao baada muda ulioapngwa kukamilka huku wakibaki katika foleni ndefu.
Kitendo cha Kamati ya maandalizi kukatisha zoezi la kuuaga mwili wa marehemu kwa sababu ya muda uliopangwa kukamilika iliwashangaza mamia ya watu waliokuwa kwenye foleni ya kusubiri kupata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho mbele ya Jeneza la Mangwea.
Zoezi hilo liloanza saa 2:30 asubuhi imesitishwa saa 6:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, na msafara ukiongozwa na Askari wa Jeshi la Polisi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwa katika Viwanja vya Leaders Club.
Barabarani Asakari wa Kikoso Cha Usalama Barabarani pia walijiapanga vizuri kuhakikisha kwamba msafara wa mwili wa marehemu unapita vizuri katika maeneo yaliokuwa yamepangwa kuelekea mjini Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr Blue alifika katika viwanja hivyo akiwa amechelewa na kukosa muda wa kuuaga mwili wa Mangwea lakini alipokutana na mashabiki wa muziki wake aliweza kusimama na kuwapa pole.
Mwili wa Mangwea hivi sasa uko safarini kuelekea Mjini Morogoro ambapo utalala nyumbani kwa mama yake na kesho uwakazi wa Mji huo pia watapata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho
ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA AKIMBAKA BINTI WA MIAKA KUMI
![]() |
Mkazi mmoja wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa amenusurika kuuwawa na wananchi baada ya kukutwa akimbaka binti wa miaka kumi. |
![]() |
Tukio hilo linaelezwa kutokea jana saa nane mchana, pale ambapo mazazi wa binti huyo alipomsikia mwanaye akilia kwa uchungu, na aliposogea kujua kulikoni, alimshuudia kijana huyo akiendelea na ubakaji jambo lililosababisha apige kelele kuomba msaada wa wananchi. |
![]() |

PICHA ZA UWANGWAJI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA LEO VIWANJA VYA LEADERS
![]() |
Baadhi ya ma super star wa bongo wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuaga. |
![]() |
Jeneza likiandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho |
![]() |
Diamond akiwa dada yake Queen Darlin |
![]() | ||||||
Diamond akimuaga Ngwair |
MADIWANI WAPENDEKEZA JINA LA MKOA MPYA LIWE MBOZI, MAKAO MAKUU YAWE VWAWA
KIKAO cha dharura cha Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Mbeya kimependekeza jina la mkoa mpya wa Mbeya liwe ni Mkoa wa Mbozi badala ya mkoa wa Rungwe kama ilivyopendekezwa na wataalamu,wenye makao yake makuu wilayani Mbozi katika mji wa Vwawa.
Wakizungumza katika kikao hicho Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya walisema kuwa azma ya kupendekeza kuwepo kwa mkoa mpya katika wilaya ya Mbozi umezingatia jiografia ya mkoa na fursa za kiuchumi zilizopo badala ya hamasa za siasa.
‘’Sisi ni madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, hatuna maslahi yoyote ya kisiasa na wilaya ya Mbozi, tumezingatia fursa za kiuchumi na jiografia ya mkoa ambayo italeta tija na maslahi kwa Taifa,’’alisema Bw. Mashauri Mbembela Diwani wa kata ya Nsalaga.
Awali katika mapendekezo hayo ambayo yaliwasilishwa na Ofisa Uchaguzi wa wilaya kwa niaba ya Kaimu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bi. Marietha Mlozi,Bw.Edward Mwaigombe alisoma taarifa ya mapendekezo ya jina la mkoa mpya kuwa ni Rungwe kama lilivyopendekezwa na wataalamu.
Bw. Mwaigombe alisema kuwa, taarifa ya wataalamu imezingatia vigezo vya idadi ya watu, ukubwa wa eneo, huduma zilizopo na mawasiliano ambayo ni mapendekezo kutoka katika kamati za maendeleo za kata 14 za Ulenje, Lwanjilo, Ikukwa, Swaya, Mshewe, Igale, Iyunga Mapinduzi, Tembela, Bonde la Songwe, Utengule Usongwe, Ilungu, Ilembo na Inyala.
Alisema kuwa kamati zilipendekeza mkoa wa Mbeya ugawanywe katika mikoa miwili ya Mbeya na Rungwe ambapo mkoa wa Mbeya wenye takwimu ya idadi ya watu 1,721,795 na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 41,544 umependekezwa kuundwa kwa wilaya za Chunya,Mbozi,Momba, ambapo makao yake makuu yanatarajiwa kuwa jiji la Mbeya.
Bw. Mwaigombe alisema kuwa mkoa wa pili ambao una takwimu ya watu 985,915 na ukubwa wa eneo wa kilomita za mraba 22,073 unatarajiwa kuundwa na wilaya za Mbarali, Rungwe,Kyela na Ileje na makao yake makuu yanatarajia kuwa katika wilaya ya Rungwe.
Aidha katika taarifa hiyo kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, ilipendekezwa kuanzishwa kwa wilaya mpya kutokana na jiografia na kuzingatia mgawanyo mpya wa mkoa kati ya wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kupendekezwa wilaya hizo zigawanywe katika wilaya tatu.
Hata hivyo katika mapendekezo ya madiwani wa halmashauri hiyo walisema kuwa mji wa Mbalizi ujigawe kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya na ujitegemee kuwa wilaya kamili.
Katika mapendekezo ya awali madiwani walipendekeza majina mawili ya mkoa wa Mbozi na Mkoa wa Songwe ambapo jina la mkoa wa Mbozi lilipitishwa na madiwani kwa kura 24 dhidi ya kura 3 ambapo baadaye majina mawili ya mkoa wa Rungwe na mkoa wa Mbozi nayo yalipigiwa kura na jina la mkoa wa Mbozi lilipita kwa kura 24 dhidi ya kura tatu za jina la mkoa wa Rungwe.
Akizungumza katika kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Bw. Mwalingo Kisemba alisema kuwa mchakato huo umekuja baada ya ushauri na mapendekezo ya kuugawa mkoa wa Mbeya ambao kwa sasa una jumla ya watu milioni 2.7 na ukubwa wa kilomita za mraba 63,617.
Tuesday, June 4, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)