
Sina 
shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye 
majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina 
lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio.
Kama 
ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao 
hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa 
style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo 
ambao bado wako shuleni.
Katika hali 
ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa 
Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza 
kuwadhibiti wale wote wenye tabia hiyo ya kuvaa mlegezo na kukatiza 
mitaani.

Sheria 
hiyo inaelekeza wavaaji wote wa suruali, kaptura, mavazi ya kuogelea na 
sketi zisivaliwe chini ya inchi 3 kutoka kiunoni mwa mvaaji.
Mayor wa 
Wildwood Ernie Troiano Jr. aliwaambia waandishi wa habari kuwa 
amechoshwa na malalamiko anayoyapata juu ya vijana wanaotembea makalio 
nje kwa kushusha suruali zao kupita kiasi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog