Facebook Comments Box

Saturday, May 25, 2013

LIVE MATCH CENTRE: BAYERN MUNICH VS DORTMUND KWA PICHA ZINAZOTEMBEA NA PICHA ZA KAWAIDA

BAYERN MUNICH NDIO BINGWA WA UEFA 2012/2013
Screenshot2013-05-25at1
Screenshot2013-05-25at1

Alskdjf_original
Robben's akifunga goli zuri
Goal3_original
Gundogan's akifunga penati
Dante_original
Faulo iliyoleta penati
Goal2_original
Goli la Bayern katika muonekana mzuri

Goal1_original
Robben akimpa pasi Mandzukic alieutia mpira kimiani

.
Screenshot2013-05-25at12
Screenshot2013-05-25at12

Robben_original
Shuti la Robben's lilizuiliwa na sura ya  Weidenfeller's.
Save_original 
Kipa wa Dortmund Roman Weidenfeller. akaonesha maajabu kwa kuokoa mchomo huu

Lewandoski_original
Shuti la Lewandowski's lilizuiliwa na golikipa Manuel Neuer.

Screenshot2013-05-25at11
Will ana Jaden Smith nao wamehudhuria mchezo huu



VIDEO: ANGALIA RAIS ALIVYOKAMATWA AKIIBA PENI




VIDEO: LIVE PERFORMANCE YA NEY WA MITEGO NA DIAMOND







HAWA NDIO WACHEZAJI WATATU WALIOSAJILIWA NA SIMBA JANA

SIMBA SC usiku wa jana imesaini wachezaji watatu wapya kwa mpigo, akiwemo mshambuliaji hatari wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Zahor Iddi Pazi ambaye msimu uliopita alikuwa anatakiwa na Yanga SC akatimkia Azam FC.
Zahoro Pazi
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema leo kwamba, mbali na Zahor anayechezea JKT Ruvu kwa mkopo akitokea Azam FC, wengine waliosajiliwa ni kipa Andrew Ntala kutoka Kagera Sugar na beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kutoka Mtibwa Sugar.
Poppe, ambaye ni Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) alisema wachezaji wote wamesaini mikataba ya miaka miwili kila mmoja.
“Bado tunaendelea na usajili wetu kwa umakini na kimya kimya. Nataka nirudie kusema kwamba, sera ya Simba SC si kusajili kutoka Yanga SC. Bali wao Yanga ndio wanasajili kwetu. 
Nashangaa jana Katibu wao (Lawrence Mwalusako) ametamba ameniziba mimi mdomo baada ya kumsaini Haruna Niyonzima,”.
“Yule ni mchezaji wao, na sisi hatujawahi kutoa tamko la kumtaka yule mchezaji. Kama alikuwa anawatia presha ili wampe fedha nyingi kwa kuwahadaa Simba wanamtaka, amefanikiwa, ila sisi hakuwa kabisa katika mipango yetu,”alisema Poppe.
Poppe amesema Simba SC wanasajili kisayansi na si kama wapinzani wao hao, Yanga SC ambao wanaingia hasara ya fedha nyingi na wanacheza pata potea.
“Sisi tulimsajili Mbuyu Twite kama yeye tu, lakini wao wakaingilia akawapa sharti wamsajili na ndugu yake (Kabange Twite), wakaingia mkenge wakasajili mtu ambaye wamemlipa fedha nyingi, lakini hawajamtumia na hakuwa chaguo lao,”.
Issa Rashid akipambana na Simon Msuva wa Yanga
“Sasa sisi hatuna ulimbukeni wa aina ile katika kusajili, tunafanya mambo yetu kisayansi, na ndiyo maana wachezaji tunaosajili wanakuwa lulu na baadaye tunawauza nje kwa fedha nyingi tunapata faida kubwa, angalia Patrick Ochan, Emanuel Okwi na Mbwana Samatta. “Biashara nzuri sana. Hatukutumia hata Sh. Milioni 100 katika usajili wao, wameingiza karibu Milioni 700, Yanga wanaweza?”alihoji Poppe.
Poppe alisema pamoja na kusaini watatu hao wapya, Simba SC imewapa mikataba wachezaji wake kadhaa chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, akiwemo Haruna Chanongo ambaye alikuwa kwenye rada za Yanga pia.
Kusajiliwa kwa watatu hao wapya, kunafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika wanne, baada ya Twaha Shekuwe ‘Messi’ wa Coastal Union kuwa mchezaji wa kwanza mpya kusajiliwa katika timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Lakini Simba SC, tayari imempoteza mchezaji mmoja, Mrisho Ngassa ambaye amesajiliwa na watani wa jadi, Yanga SC.

SOURSE: BIN ZUBEIRY

PICHA: SHABIKI WA YANGA ANAELIA YANGA IKIFUNGWA AKIONESHA TIKETI YAKE YA KUANGALIA FAINALI YA UEFA LEO USIKU

#UEFA Shabiki Steven wa Yanga nae katisha!! atachekia mechi Golden Tulip leo usiku, nitatoa zawadi ya vocha kwa watu watano wa mwanzo watakaopatia kwa kuniandikia hapa, anza sasa hivi mtu wangu
Yule shabiki wa Yanga maarufu kama mzee wa uungwana akifurahi na tiketi yake ya kuangalia mechi ya Uefa leo kwenye hoteli ya Golden Tulip


JOSE MORINHO AKUBALI MKATABA WA MIAKA MINNE CHELSEA

Mitando mbalimbali maarufu ya Uingereza imeripoti kuwa Kocha JOSE MOURINHO atakwenda uingereza tarehe 2 mwezi wa 6 kwa ajili ya kutia saini mkataba wa miaka minne ambao utakuwa na thamani ya Paundi 250,000 kwa wiki.

Tajiri wa Chelsea amemuhakikishia kuwa hizo fedha zinazokaribia paundi milioni 50 zipo kwa ajili ya mkataba huo. Hilo litamfanya haraka baada ya mechi ya Real Madrid na Osasunaambayo ndio mechi ya mwisho kwa Real Madrid msimu huu kutompotezea muda kocha huyo maana baada ya mechi hiyo atapanda ndege na kwenda uingereza kwa ajili ya mkataba huo. Katika safari hiyo ataongozana na kocha wa viungo Rui Faria na kocha wa magolikipa Salvino Louro.


Friday, May 24, 2013

BREAKING NEWS: AMRI KIEMBA ASAINI YANGA

 
WAKATI Haruna Niyonziam akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, habari zilizotufikia hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na mtandao huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema Kiemba amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao huu unaahidi kuwasiliana na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini katika kambi ya Taifa Stars kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake kwa Yanga.
Kiemba aliwahi kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA


M23 KUIVAMIA TANZANIA; WANANCHI WA KAGERA WATAHADHARISHWA

Serikali ya Mkoa wa Kagera imewatahadharisha wananchi wake kuepukana na wageni wasiowafahamu kwenye maeneo yao kutokana na tishio la kikosi chaM 23 cha nchini Congo DRC kinachotishia kuivamia Tanzania...
Kumekuwa na mapigano  makali  kati  ya waasi waM23  na  vikosi vya serikali  nchini  Congo ambako jeshi letu lipo huko...
Waasi  hao  wametishia  kuivamia  Tanzania  muda  wowote  ili  kulipiza  kisasi.Miongoni mwa mipaka ambayo iko wazi  ni Kagera, na hii ndo sababu iliyopelekea  serikali ya Mkoa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla....


HATIMAYE NIYONZIMA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI

Miaka miwili zaidi; Haruna  Niyonzima kushoto akiwa na mwanawe, ameongeza miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga. Hapa alikuwa anapokea Medali ya ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kutoka kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga
HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.
Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana.
 Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.
 Mwalusako amesema kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili.
Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.
Naye Niyonzima amesema anawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu ya Yanga Abdallah BinKleb amesema palikua na propaganda nyingi juu ya Niyonzima, lakini ukweli ndio huu Niyonzima ataendelea kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka miwili.
"Tunautambua mchango wake alioutoa kwa miaka mwili kwani ameweza kutupatia vikombe viwili vya Ligi Kuu ya Vodacom na Kombe la Kagame hivyo tumemuongezea mkataba wa miaka miwili tena ili aendelee kutoa mchango wake na kuisadia timu katika michezo ya kimataifa" alisema BinKleb
SOURSE: BIN ZUBEIRY


Thursday, May 23, 2013

MAJAMBAZI WAMELIVAMIA HILI GARI NA KUPORA PESA LEO




Matundu matatu ya risasi katika kioo cha gari lililovamiwa na majambazi.

Wanausalama barabarani wakichukua taarifa eneo la tukio.

Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya VITZ N a kuwajeruhi watu wawili wenye asili ya asia na kupora kiasi cha fedha ambacho bado thamani yake haijafahamika mara moja.


KIBONZO: VURUGU ZA MTWARA

Picture


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU