Facebook Comments Box

Thursday, April 18, 2013

BI KIDUDE AZIKWA NA UMATI WA WATU ZANZIBAR


Jeneza la bibi likielekea msikitini kwa ajili ya kuswaliwa
 
Jeneza lenye Mwili wa Msanii mkongwe wa Muziki wa  Taarab, Marehem Fatma Bint Baraka Khamis(Bi Kidude) likitolewa katika msikiti wa Mwembeshauri aliposwaliwa mchana wa leo kabla ya kwenda kuzikwa.

 Taratibu za Mazishi zikiendelea kama inavyo onekana katika picha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) Katika makaburi ya Kitumba wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq akiweka udongo.
Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu bi Kidude,  Zanzibar
Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi)
Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude

Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude
Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani







Wednesday, April 17, 2013

HII NDIO SABABU YA KIFO CHA BI KIDUDE

Kidude
Mjukuu wake aitwaye Omar ameiambia Bongo5 kwa simu muda mfupi uliopita kuwa Bi. Kidude alikuwa amelazwa kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe kwenye kongosho.
“Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu akachukua roho yake,” amesema Omar.
 Omar amesema mazishi yanaweza kufanyika kesho. Mungu ailaze roho ya marehemu Fatuma binti Baraka mahala pema peponi. Amen.





HEBU SIKILIZA TUSI ALILOTUKANA HUYU MBUNGE LEO BUNGENI

Bunge letu linaelekea wapi? hebu sikiliza hili tusi alilotoa huyu mbunge leo ndani ya bunge.







KIBONZO: KIPANYA AKIZUNGUMZIA MATUSI WANAYOTUKANANA WABUNGE NDANI YA BUNGE




BI KIDUDE AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia hivi punde amefariki dunia. Habari hizo zimepatikana kutoka moja ya Tv kubwa ya burudani Afrika Mashariki na kuenezwa vile vile na watu mbali mbali mashuhuri kama tulivyo ziweka hapo chini.Inna Lillah wa Inna Illayhi Rajiuun. 



DR BILAL AFUNGUA RASMI MKUTANO WA WANASAYANSI WA AFRIKA


Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali akifungua rasmi Mkutano wa Pamoja wa Kimataifa wa Watafiti Wanasayasi Afrika ulioandalia na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS) ya Afrika Kusini. Kushotoni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Mwele Malecela. Mkutano huo wa siku nne unafanyika Jijini Arusha. 

Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na Dk Martha Lemnge mara baada ya kuwakabidhi tuzo zao hii leo. 

Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na Dk Martha Lemnge mara baada ya kuwakabidhi tuzo zao hii leo. Kulia ni Mkurugenzi wa NIMR, Dk Mwele Malecela. 


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu TanzaniaNIMR), Dk Mwele Malecela akisoma hotuba yake.





Badhi ya Watafiti Wanasayansi kutoka Taasisi zaidi ya 35 barani Afrika wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa NIMR wakati wa hotuba yake ya ukaribisho. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS), Mark Rweyemamu akisoma risala yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Jijini Arusha. 

Viongozi wa NIMR na Watafiti mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa SACIDS. 

Mkurugenzi wa OHCEA, Japhet Kilewo akitoa hotuba yake. 

Meza kuu ikifuatilia kwa ukaribu Hotuba ya Mkurugenzi wa OHCEA. 

Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dk Ahmed Hamdy akizungumza na Wanasayansi watafiti. 

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid nae alisoma Hotuba ya Wizara na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo. 



Wakuu wa Taasisi za kitaifa na Kimataifa pamoja na wanasayansi watafiti wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.



Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela wakizindua rasmi awamu ya nne ya Vipaumbele vya Tafiti za Afya kwa mwaka 2013-2018.


Pia Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzindua Mpango wa Afya Moja nchini Tanzania 

Aidha Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal pia alizindua Mpango wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS).


WABUNGE WANNE WAFUKUZWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

Chama tawala nchini Uganda cha National Resisitance Movement-NRM- kimewafukuza baadhi ya wanachama wake wanne, wote wakiwa ni wabunge, kwa kile kilichoitwa utovu wa nidhamu.

Mbunge mwingine yeye amesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu kwa sababu za ulevi.

Katibu mkuu wa chama hicho Amama Mbabazi anasema hii kwa tafsiri yake inamaanisha kuwa wabunge hao wamepoteza viti vyao, jambo ambalo wahusika wanapinga.

Katibu mkuu wa chama tawala cha NRM na wakati huo waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi, ametangaza maamuuzi ya kamati kuu ya chama hicho kuhusu majaliwa ya wabunge wanne waliopewa jina la ‘wabunge waasi’ kutokana na misimamo yao dhidi ya masuala mbalimbali katika chama hicho.

Mbabazi alitoa kauli hiyo na kusema, “Muhammad Nsereko afukuzwe kutoka NRM;kuwa Theodor Sekikubo afukuzwe kutoka NRM; kuwa Barnabas Tinkasimire afukuzwe kutoka NRM; kuwa Wilfred Nuwagaba wamefukuzwe kutoka NRM; na kuwa Vicent Kyamadidi Muzuni asimamishwe uana chama wa NRM kwa muda wa miezi mitatu.”

Wabunge wanne waliofukuzwa kutoka chama: Nsereko; Sekikubo; Tinkasimire pamoja na Niwagaba wamekuwa wakipinga na kukosoa saana uongozi wa sasa wa chama hususan kutokana na madai ya ufisadi dhidi ya vigogo wa chama.

Na wanasema hatua hii ni ya kuwaandama kisiasa kwa kusema ukweli dhidi ya wanachoita uongozi mbaya. Hatua ya kuwafukuza wanachama hao , inasekena ni kutokana na utovu wa nidhamu.

Wabunge hao walishtakiwa katika kamati ya nidhamu ya chama na kukabiliwa mashataka saba: kuwapigia debe wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mdogo; kupaka matope wagombea rasmi wa chama cha NRM wakati wa uchaguzi mdogo; kutoa madai ya uongo kwa vombo vya habari dhidi ya chama cha NRM; kutumia majukwaa haramu, kama vile vyombo vya habari na mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kuzungumzia masuala yanayowakera;kujihusisha katika uundaji wa genge ndani mwa NRM; matumizi ya lugha chafu;na mwisho kukaidi kamati ya nidhamu ya chama.Wote licha ya kuwaita kufika mbele ya kamati hiyo kujieleza walipinga.

Hii ndiyo mara ya kwanza tangu mfumo wa vyama vingi kuanza tena mwaka wa 2006, chama cha NRM kufukuza wanachama wake.

Na hii imezusha tafsiri tofauti kwa wabunge wanaofukuzwa chama.Katibu mkuu wa NRM anasema kuwa hii inamaanisha kuwa wamepoteza viti vyao vya ubunge.

Mbabazi aliongeza kusema kuwa ''Kulingana na sheria za Uganda, hususan kifungu 83 cha katiba ya taifa ni kuwa mtu anaweza kuwa mbunge pindi tu ikiwa amechaguliwa kama mbunge wa kujitegemea,au ikiwa amechaguliwa baada ya kuungwa mkono na chama Fulani,au ni waziri,au kama mwanajeshi.''

Hakuna njia nyingje ile. Wabunge hao wanasema kuwa katiba haikubali mbunge yeyote kubadili chama bungeni.Ikiwa mtu atapoteza uungwaji mkono wa chama chake hii ina maana kuwa amepoteza kiti chake.

Lakini hilo limepingwa na mbunge muathiriwa na tena wakili, Wilfred Niwagaba.

Niwagaba alisema ''Ikiwa anadhani kwa kutusimamisha au kutufukuza uanachama ina maana kuwa tunapoteza viti vyetu,nasikitika sikubaliani na tafsiri hiyo.Hakuna hata mmoja wetu ameondoka kutoka chama kwa hiari.''Hata hivyo mwenzao Vincent Kyamadidi amesimamishwa uanachama kwa muda kutokana na madai kuwa alilewa na kujaribu kupigana hadharani jambo ambalo linakwenda kinyume na maadili ya chama.

Aidha yeye alipoita kujieleza alifika mbele ya kamati hiyo.

Bado kuna vuta ni kuvute kuhusu majaliwa ya wabunge wanne, ikisemekana wamekwenda mahakani kupinga kufukuzwa kwao.

Tuesday, April 16, 2013

VIDEO YA SPIKA WA BUNGE AKIKEMEA WABUNGE KUTUKANANA NDANI YA BUNGE

">

ANGALIA PICHA YA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA NAY WA MITEGO NA DIAMOND WIMBO MUZIKI GANI

Ngoma hiyo iliyofanywa na Producer Mr. T Touch ikijulikana kama MUZIKI GANI imeanza matengenezo hayo kwa kasi ...
Wimbo huu ambao unaonekana kuendelea kupendwa sana na mashabiki pamoja na kupondwa na baadhi ya watu, umeanza kurekodiwa video yake ambapo moja ya shot zake ni hii pichani inayowaonesha na warembo wakionekana kama kucheza mchezo kamari ...
Let's wait kuona Ney na Diamond wanatuletea nini kwenye video hii.


USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU (FRIJI)

Na Hassan Bilal Ka'bange
Watu wengi watashangaa kwa nini wasiweke ndizi kwenye jokofu zao. lakini baada ya kusoma makala hii watajua kwanini haitakiwi kuweka ndizi kwenye jokufu na wataziangalia ndizi zao tofauti na walivyokuwa wakiziangalia zamani.
Ndizi zina sukari halisi ya aina tatu sucrose (Sukrosi), Fructose (Fruktosi) na Glucose (Gluktosi) ambazo zimeungana na fiber. Kwa hali hii ndizi zinakupa nguvu halisi na nzuri kwa ajili ya mwili wako.
Tafiti zinaonesha ndizi mbili zinatosha kukupa nguvu za kutosha kufanya kazi ngumu kwa muda wa dakika 90. Kwa hili siwezi kushangaa kuona ndizi kuwa ndio tunda linaloongoza kuliwa na wanamichezo wakubwa duniani.
lakini nguvu sio kitu pekee tunachokipata katika ndizi ambacho kinatupa umakini. Ndizi bado inatupa nguvu ya upambanaji na kinga dhidi ya magonjwa mengi sana. Na hilo ndilo linalofanya leo hii ndizi niisisitize iwe katika mlo kamili wa kila mwanadamu. Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ambayo ndizi inaweza kukukinga na kukutibu kwayo.

KUONDOA MSONGO WA MAWAZO:
kulingana na  tafiti fupi iliyofanya kwa wagonjwa wengi walio katika msongo wa mawazo yaani kitaalam DEPRESSION wengi wao wameonesha kupata nafuu na ahuweni baada ya kula ndizi. Hii inatokana na ndizi kuwa na kemikali ijulikanayo kama Tryptophan ambayo ni asili ya ptotini ambayo mwili huweza kuibadilisha na kuwa homoni ya Serotonin (serotonini) ambayo humfanya mgonjwa kutulia, kupata ahueni ya muhemko na kumfanya apate furaha.
Vilevile ndizi ina vitamini B6 ambayo husahihisha sukari ndani ya damu ambayo huleta athari katika mhemko.

KUONGEZA WINGI WA DAMU:
Ndizi ina madini chuma mengi, kwa muono huo ndizi huleta uchochezi katika utengenezwaji wa chembechembe za damu ambazo hujulikana kwa jina la Hemoglobin (himoglobini) hivyo husaidia ongezeko la damu mwilini.

KUONDOA SHINIKIZO LA DAMU:
Ndizi ni tunda la ajabu sana(unique) linalopatikana katika ukanda wa ki tropika ambalo lina madini ya potasiamu (Potassium) mengi na bado likiwa na chumvi kidogo, Hivyo inalifanya kuwa madhubuti katika kupambana na shinikizo la damu sana. Mamlaka ya Chakula na dawa ya Ameriaka ( US Food and Drug Authority) wameruhusu viwanda vya ndizi kuweka nembo zinazo onesha kuwa chakula hicho kinaweza kupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu na kiharusi.


KUONGEZA UWEZO WA AKILI WA KUFIKIRI NA KUKARIRI:
Wanafunzi 200 wa shule ya upili ya  Twickenham ya uingereza walisaidiwa ufaulu kwenye mitiani yao kwa kula ndizi wakati wa kifungua kinywa na wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana kwa ajili ya kuongeza nguvu zao za kufikiri. Hii inaweza isieleweke vizuri lakini tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa madini ya potasiam (Potassium) yaliyopo kwenye ndizi yanasaidia uwezo wa kusoma kwa kufanya macho kuwa hai muda wote (Makes pupils more alert).

KUONDOA MAUMIVU YA TUMBO:
Watu wengi wamekuwa wakilalamika maumivu ya tumbo na kupata haja ngumu. Ndizi ina fiber nyingi ambazo husaidia kuweka sawa mwenendo wa utumbo na husaidia matatizo ya haja ngumu.

KUONDOA MNING`INIO:
Moja ya njia rahisi na nyepesi wa kuondoa mning`inio ni kutengeneza mkorogo wa ndizi na maziwa (Banana milkshake) ambao itahitajika kuongeza na asali kidogo kwa ajili ya kuongeza utamu. Pamoja na ladha nzuri na utamu utakao upata mkorogo huu wa ndizi utakusaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini wakati maziwa yatasafisha na kukuongezea maji mwilini.

KUONDOA KILUNGULIA:
Ndizi ina vimelea vya asili ambavyo hupambana na kilungulia. Kwa hiyo kama una matatizo ya kilungulia acha kula majivu ambayo hata haujui miti iliyotumika kama ina sumu hau hapana chukua ndizi moja ikuondolee matatizo.

KUONDOA HOMA ZA ASUBUHI:
Kula ndizi katikati ya kila mlo hufanya ndizi kusahihisha kiwango cha sukari mwilini na kukuondolea homa za asubuhi.

KUKUKINGA DHIDI YA UVIMBE WA KUNG`ATWA NA MBU:
Kabla ya kwenda dukani na kununua madawa ambayo yana madhara makubwa katika mwili wako na mazingira hebu chukua ganda la ndizi ule upande wa ndani jikunie/paka eneo ulilong`atwa na mbu. Watu wengi wamepata matokeo mazuri ya upunguzwaji wa muwasho na uvimbe unaotokana na kung`atwa na mbu..

KUKUONDOLEA MATATIZO YA NEVA ZA FAHAMU (NERVES):
Ndizi ina vitamini B nyingi ambayo hukusaidia kufanya neva zako za fahamu kuwa sahihi na salama.

KUKUONDOLEA ATHARI ZA KUPATA VIDONDA VYA TUMBO:
Ndizi ikitumika kama chakula hukuondolea athari za kupata vidonda vya tumbo kwa ajili ya umbo lake laini na murua. Vilevile husaidia kurekebisha (Neutralize) wingi wa asidi (acidity) na kupunguza mkwanguo kwa kuweka kava katika utumbo.

KUREKEBISHA JOTO MWILINI:
Tamaduni nyingi zimekuwazikiona ndizi kama kitulizo cha mhemko na kimwili wa wamama wajawazito kwa mfano nchini Thailand wamama wajawazito hula ndizi ili kuhakikisha watoto wao wazaliwe na joto sahihi. Kwetu hasa Maeneo ya Mbeya, Kagera na Kilimanjaro wamama wajawazito hupewa mkorogo wa ndizi na nyama maarufu kama Mtori ili waweze kunyonyesha salama na kurudisha afya yao na kuwakinga na magonjwa.

Ndizi ni dawa halsi ya magonjwa mengi. Ukitaka kufananisha na Tufani (apple) ndizi ina ptorini mara nne zaidi ya tufani ina sukari mara mbili ya tufani, ina madini ya fosforasi (Phosphorus) mara tatu ya tufani, ina mara tano zaidi vitamini A na madini ya chuma na ina mara mbili zaidi ya madini mengine. Bado ikiwa ni tajiri wa madini ya potasiamu na mengine.
Ni wakati sasa wa watanzania wenzangu kulipenda tunda hili na kulila ipasavyo. Na kwasasa sipati shida sana kuona nyani anavyo furahi na kuruka ruka unapomtupia ndizi inawezekana anajua thamani yake katika mwili wake.

TULE NDIZI ITUJENGEE MIILI YETU NA KUTUKINGA NA KUTUTIBU  MAGONJWA




HUU NDIO UKUBWA WA HARD DISK DRIVE YA KWANZA NA YA SASA




 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU