Facebook Comments Box

Friday, April 5, 2013

POLISI ZANZIBAR WAKANA UPELELEZI WA KESI YA PADRI MUSHI KUFANYWA NA FBI



BAADA ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DDP) kulitaka Jeshi la Polisi kumwachia mtuhumiwa Mussa Omar Makame kutokana na ushahidi kutojitosheleza, jeshi hilo sasa limeingia kwenye mkorogano.

 Katika mahojiano, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa A. Mussa, alikanusha jeshi la polisi kushirikiana na kikosi cha upelelezi cha Marekani (FBI) ili kumkamata Makame.

Kauli yake inakinzana na ile aliyoitoa Machi 23, mwaka huu aliposema uchunguzi huo ulikuwa ukifanywa na makachero wa polisi kwa kushirikiana na wapelelezi kutoka Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo.

Katika mkorogano huo wa taarifa kuhusu Makame, tamko rasmi la Jeshi la Polisi nchini lililotumwa kwa vyombo vya habari halikumtaja mtuhumiwa kwa jina likidai uchunguzi unaendelea lakini Kamishna Mussa alimtaja kuwa ni Mussa Omar Makame.

Kamishna Mussa jana alilieleza kuwa licha ya DPP kusema Makame hana hatia, wataendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.
“Sisi tutaendelea kumshikilia hata kama DPP hakuridhika na upelelezi tuliofanya, tuna taratibu mbalimbali ambazo si lazima kuzitaja kwa sasa,” alisema.

Alipotakiwa kufafanua kama ni kweli FBI hawakushirikiana nao katika uchunguzi huo, kamishna huyo aliomba apigiwe simu baadaye kwa madai kuwa alikuwa na kazi, lakini alipotafutwa tena hakupokea simu. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, Isaya Mungulu, alipotakiwa kuzungumzia mkorogano huo wa kauli, alidai apigiwe Kamishna wa Zanzibar ndiye anayejua vizuri.


Thursday, April 4, 2013

ANGALIA UWANJA WA YANGA UTAKAVYO KUWA BAADA YA UJENZI KUKAMILIKA


Ramani ya uwanja mpya wa klabu ya Yanga - Kaunda Stadium unavyoekana kwa ndani
















Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi akinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG  Zhang Chengwei David amesema upembuzi akinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja wa mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.
Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.
Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000.
Katika uwasilishaji huo wa makadirio ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa kukamilisha zoezi la upembuzi akinfu mapema ambapo leo wamepata fursa ya kujionea na kujua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo. 
Kufukwe alisema wamepewa nafasi ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mktaba kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda.
Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za ujenzi wa uwanja, Kufukwe alisema ujenzi wa uwanja wa mpya utajengwa na wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga.
Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.
Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maaalumu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.
Ramani ya mchoro wa Uwanja mpya wa Kaunda unavyoonekana kwa nje





AMANI YETU INACHEZEWA SANA

Picture

SAKATA LA MAUAJI YA PADRI MUSHI: DPP HAJAONA USHAHIDI WA KESI YA MAUAJI

DPP wa Serikali Ibrahim Mzee asema hajaona ushahidi ambao ungemuwezesha kumshitaki kijana Omari alituhumiwa kwa mauwaji ya Padri Mushi.

 Na kwa upande wa Mahakama pia umelitaka Jeshi la Polisi kumfikisha mtuhumiwa huyo Mahakamani siku ya Jumatatu na waeleze vielelezo tosha kwanini wamemchelewesha­ kumpeleka mahakamani wakati wanajua kuwa mtuhumiwa hupaswa kukaa kituo cha Polisi kwa muda wa masaa 24 tu na baadae kufikishwa mahakamani.

Wednesday, April 3, 2013

ANGALIA VURUGU YA TUNDUMA




VURUGU ZATOKEA TUNDUMA JUU YA NANI ACHINJE

Ghasia zinazoendelea katika mji wa Tunduma ulioko mkoani Mbeya zimechochea uharibifu kijamii. Tunduma haiko katika hali nzuri.
 Vurugu kama hizo ziliwahi kutokea mjini Mwanza na kuhusisha wamumini wa imani ya kikristo na Kiislamu. Mauaji yalitokea na serikali ilifanya juhudi kuwakamata wahusika.

Ni kwamba inaelekea hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu uchinjaji bado haijaeleweka, hivyo wakristo bado walikuwa na msuguano na wenzao juu ya nani achinje.

Tamko la Polisi lilisema waislamu waendelee kuchinja sasa leo alfajiri vijana wa kikristo walienda machinjoni na kumgawia kichapo cha kutosha mchinjajiwa kiislam ambaye alifanikiwa kutoroka.

Baada ya hapo wakristo nasikia ndiyo wakaanza hizo fujo ikiwemo pamoja na kufunga barabara, kuharibu msikiti, kubomoa nyumba ya polisi mmoja aliyejenga uraiani, wameandamana na biblia mikononi kudai haki ya kuchinja.

Polisi wa Tunduma kazi imewaelemea na ikabidi nguvu itoke mkoani na RPC yupo huko sasa hivi. Juzi kanisani Padre mmoja alitoa kauli kuwa kama hawa watu wanataka kuchinja basi watuchinjie na kitimoto.

Raia ilibidi wakimbilie mahakamani kwa kuona kwamba ndiyo sehemu pekee ya usalama kwao, hivyo ikalazimu mahakama kuhairishwa ili kuepusha balaa. Kale kamchezo kakuchoma matairi na kufunga barabara kakawa ndiyo mchezo wa kawaida.

FILAMU YA MWISHO YA KANUMBA KUZINDULIWA LEADERS CLUB APRIL 12, 2013 BURE








Familia ya Kanumba inawakaribisha katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha marehemu Steven Kanumba itakayofanyika Leaders Club  Jumapili hii tarehe 12 /04/  2013 kuanzia saa 8 mchana.

Kutakuwa na uzinduzi wa muvi ya mwisho kufanywa na marehemu. Pia itaoneshwa kwa mara ya kwanza preview ya muvi iitwayo After death(Never happened before) iliyoandaliwa na Jackline Wolper kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba.Kutasindikizwa na Twanga Pepeta na wachekeshaji maarufu Tanzania.KIINGILIO NI BURE. MSIKOSE TUMUENZI NDUGU YETU.

 Filamu mpya ya ''Love & Power'' ambayo ndio baadhi ya kazi za mwisho za msanii hayati Steven Charles Kanumba, ambapo yumo pia marehemu Sharo Milionea, inatarajiwa kuingia sokoni baada ya msambazaji wa filamu hiyo kuikamilisha na kusema kuwa filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwezi April baada ya kuzinduliwa kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni… Filamu ya ''Love & Power'' ni kazi ya pekee kuigizwa na msanii huyo kabla ya umauti kumfika, ni filamu aliyorekodi siku za mwisho kabisa… Filamu hiyo ambayo wengi wanasema marehemu Kanumba alijitabiria kifo chake, itazinduliwa sambamba na kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwake, April 7 2012… Akizungumza kupitia EATV hii leo, mdogo wa marehemu Kanumba ambaye pia ni kiongozi wa ofisi ya ''Kanumba The Great'' iliyopo Sinza-Mori, Seth Bosco, alisema zaidi ya waigizaji 10 kutoka Ghana wanatarajiwa kuwepo siku hiyo… Alisema mbali na waigizaji hao wa Ghana, pia rafiki wa marehemu, ambaye ni muigizaji maarufu barani Afrika kutoka Nigeria, Ramsey Noah pia anatarajiwa kuwepo siku hiyo ya uzinduzi… Akizungumzia ratiba ya siku hiyo, Seth Bosco alisema itaanzia nyumbani kwa marehemu, baada ya hapo wataelekea makaburini Kinondoni na baadaye Leaders Club kwa ajili ya uzinduzi huo.


VIWANGO VIPYA VYA NAULI KWA MUJIBU WA SUMATRA.


IMG_6840
 
Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA Athman Kilima akizungumza na waandishi wa habari  katika makao makuu ya taasisi hiyo wakati akitangaza kupanda kwa viwango vya nauli ya mabasi ya mikoani na Daladala.
 
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.
 
SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji. Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe. 
 
Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C, Happy Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.
 
Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.
 
Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.
 
Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16 Cha Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma, faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za huduma inayotolewa.
 
Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 24.46%.
 
Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa mabasi ya kawaida, 16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi ya daraja la juu.
 
Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:
  1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam

Umbali wa NjiaKiwango Kipya cha NauliMfano wa Njia
Kilomita kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)Sh 400/=Ubungo – Kivukoni
Kilomita kati ya 11 – 15Sh 450/=Mwenge – Temeke
Kilomita kati ya 16 – 20Sh 500/=Tabata Chang’ombe – Kivukoni
Kilomita kati ya 21 – 25Sh 600/=Pugu Kajiungeni – Kariakoo
Kilomita kati ya 26 – 30Sh 750/=Kibamba – Kariakoo
Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam. Majedwali hayo yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz.
 
Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.
 
2.Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu 
 
Daraja la BasiNauli ya zamani kwa km-abiriaNauli mpya kwa km-abiriaMfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia
Basi la Kawaida kwa njia ya lamiSh 30.67Sh 36.89DSM–Mbeya Km 833Sh 30,700
Basi la Kawaida kwa njia ya vumbiSh 37.72Sh 46.11S/wanga-KigomaKm 551Sh 25,400
Basi la hadhi ya kati (Semi LuxurySh 45.53Sh 53.22DSM–Mwanza Km 1,154Sh 61,400
Basi la hadhi ya juu (Luxury)Sh 51.64Sh 58.47DSM–Arusha Km 616Sh 36,000
Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:
    1. Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za safari
    2. Wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli
    3. Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
    4. Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora.
       
      Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo:
    1. Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
    2. Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyote kwa abiria
    3. Kutokutumia wapiga debe
    4. Wafanyakazi wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.
Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu na Mamlaka zingine kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango cha juu.
 
A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013


BAADA YA KUWACHANA CLOUDS FM SASA LADY JAYDEE AWACHANA WASANII WA THT


jide na ben
Wengi mnafahamu anachokiandika Lady Jaydee siku za hivi karibuni na sasa kibao kimemuendea Linah na Ben Pol.
Lady Jaydee anadai wasanii wa THT wamemsaliti kwa kile anachodai walikatazwa kwenda kuperform Nyumbani Lounge licha ya kuwalipa advance.
“Linah na Ben Pol mnabisha hamkukatazwa? Nisalitini ila hamtapata faida mtatoka kapa pia,” ametweet Jide.
Shutuma hizo zimepolekewa kwa hasira na Ben Pol aliyemjibu Jaydee:
“Hiyo show kulikuwa na wengine pia wakuperform je wali perform? kama nililipwa nanikashindwa ku show up, mbona sidaiwi?? Tafakari.”
Aliongeza, “Ben Pol hana muda wa maneno na majungu. Ombi langu ni mmoja kwako. Put me out of your business. PERIOD.”
“Don’t talk about things you don’t know about. DON’T.”
“Ukiwaza kutumia akili kamwe huwezi kukosea, ila utakapotumia hisia lazima ujikanyage somewhere. Nimekua vya kutosha #Trustme,” alimalizia Ben.
Unazungumziaje hiki kinachooendelea sasa na athari yake kwenye muziki wa Tanzania. Maoni yako tafadhari.

MAHAKAMA YAFUTA KESI YA VIONGOZI WA UAMSHO


Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe imeifuta kesi moja inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), kutokana na kuchukua muda mrefu bila ushahidi wake kukamilika.
Hakimu Ame Msaraka Pinja alisema jana kuwa, anaifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 209 cha makosa ya jinai.
Washtakiwa wa kesi hiyo ambayo ilikuwa ni moja kati ya tatu zinazowakabili ikiwa kwenye Mahakama hiyo na nyingine Mahakama Kuu, walikuwa wanakabiliwa na kesi ya kuhatarisha amani kwa kutoa lugha kali.
Ilipotajwa mara ya mwisho, Machi 19 mwaka huu upande wa mashtaka ulidai kuwa, upelelezi  haujakamilika na mawakili wa utetezi walimwomba hakimu kuifuta kwa vile washtakiwa wako ndani muda mrefu.
Wakili wa washtakiwa hao, Salum Toufik na Abdallah Juma walimwomba hakimu kutokana na taratibu za Mahakama hususan makosa ya jinai, kesi inapofikia  miezi mitatu na kuendelea bila  upelelezi kukamilika inapaswa kufutwa.
Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Khamis Jafar waliomba Mahakama kuwapa muda zaidi kutokana na kuchukua kipindi kirefu bila upelelezi kukamilika.
Washtakiwa hao ni Masheikh Farid Hadi, Mselem Ali, Mussa Juma, Azza Khalid Hamdan, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari. Washtakiwa hao bado wanakabiliwa na kesi iliyopo chini ya Hakimu wa Wilaya, Khamis Rashid na washtakiwa wanne wapo nje kwa dhamana, huku watatu wakiwa rumande kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine Mahakama Kuu.  Washtakiwa watatu ambao walikwenda katika kesi hiyo wakitokea rumande ni Masheikh Farid, Juma Suleiman na Mussa Juma.


MSHABIKI WA SIMBA ANAPOMWAGA KIZUNGU

Picture

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU