
Familia ya Kanumba inawakaribisha katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha marehemu Steven Kanumba itakayofanyika Leaders Club Jumapili hii tarehe 12 /04/ 2013 kuanzia saa 8 mchana.
Kutakuwa na uzinduzi wa muvi ya mwisho kufanywa na marehemu. Pia itaoneshwa kwa mara ya kwanza preview ya muvi iitwayo After death(Never happened before) iliyoandaliwa na Jackline Wolper kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba.Kutasindikizwa na Twanga Pepeta na wachekeshaji maarufu Tanzania.KIINGILIO NI BURE. MSIKOSE TUMUENZI NDUGU YETU.
 Filamu
 mpya ya ''Love & Power'' ambayo ndio baadhi ya kazi za mwisho za 
msanii hayati Steven Charles Kanumba, ambapo yumo pia marehemu Sharo 
Milionea, inatarajiwa kuingia sokoni baada ya msambazaji wa filamu hiyo 
kuikamilisha na kusema kuwa filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mwezi
 April baada ya kuzinduliwa kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni… 
Filamu ya ''Love & Power'' ni kazi ya pekee kuigizwa
 na msanii huyo kabla ya umauti kumfika, ni filamu aliyorekodi siku za 
mwisho kabisa… Filamu hiyo ambayo wengi wanasema marehemu Kanumba 
alijitabiria kifo chake, itazinduliwa sambamba na kumbukumbu ya mwaka 
mmoja tangu kufariki dunia kwake, April 7 2012… Akizungumza kupitia EATV
 hii leo, mdogo wa marehemu Kanumba ambaye pia ni kiongozi wa ofisi ya 
''Kanumba The Great'' iliyopo Sinza-Mori, Seth Bosco, alisema zaidi ya 
waigizaji 10 kutoka Ghana wanatarajiwa kuwepo siku hiyo… Alisema mbali 
na waigizaji hao wa Ghana, pia rafiki wa marehemu, ambaye ni muigizaji 
maarufu barani Afrika kutoka Nigeria, Ramsey Noah pia anatarajiwa kuwepo
 siku hiyo ya uzinduzi… Akizungumzia ratiba ya siku hiyo, Seth Bosco 
alisema itaanzia nyumbani kwa marehemu, baada ya hapo wataelekea 
makaburini Kinondoni na baadaye Leaders Club kwa ajili ya uzinduzi huo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog

