Facebook Comments Box

Saturday, February 9, 2013

LIVE MATCH CENTRE:FULL TIME SIMBA SC 1 - 1 JKT OLJORO



Mpira umemalizika Simba 1-1 JKT Oljoro

Mpira unaweza isha muda wowote na matokeo bado 1kwa1.Zimeongezwa dk 2


Dk ya 42 kipindi cha pili simba wanapoteza nafasi ya kupata bao la ushindi


Dk 37 kipindi cha pili Jkt oljoro wanakosa goli la wazi.

Dk ya 28 kipindi cha pili, simba wanafanya mabadiliko Edward christopher anaingia na anatoka MudeJkt oljoro wanakosa goli la wazi na wanafanya mabadiliko kwa kumtoa Esau.

Ngasa ameingia kuchukua nafasi ya Rashid

Jkt wanasawazisha bao kufuatia uzembe wa beki ya simba.

JKT OLJORO wanakosa goli la wazi na wanafanya mabadiko ya mchezaji.

Mchezaji wa JKT anapewa kadi ya njano kwa kumkwatua Kazimoto.

Kipindi cha pili kimeanza hakuna mabadiliko yoyote.

Mashabiki wanaodhaniwa wa simba wanawashambulia watu waliovaa nguo zinazodhaniwa za CCM.

Dk 38 Oljoro wanalishambulia sana lango la Simba kwani wanaonyesha kuwakamata vilivyo

Hadi dk ya 34 simba wanaongoza goli moja lililofungwa na Kazimoto kwa shuti kali umbali wa mita 30

Paul Ngalema ameumia vibaya na kutolewa uwanjani ameshindwa kuendelea na mchezo

Dk ya 29 JKT OLJORO wanakosa goli la wazi ktk shambulizi baada ya mpira kumtoka mikononi na JKT wakazubaa.

Kikosi cha Simba kinachoanza leo dhidi ya JKT Oljoro


KASEJA, CHOLLO, NGALEMA, KAPOMBE, KEITA, JONAS, KIEMBA, MUDDE, RASHID ISMAIL, KAZIMOTO na Haruni CHANONGO.


TAARIFA YA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA CCM



Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi itafanya Mkutano wake wa kawaida kuanzia tarehe 10 -11 /02/2013. Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.   
Wajumbe wa NEC wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma leo tarehe 9/02/2013,kwa ajili ya kikao hicho.   
Pamoja na mambo mengine kikao hichi kitatanguliwa na Semina ya siku mbili kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.   
 Lengo la Semina hii ni kuwaongezea Wajumbe uelewa kuhusu masuala ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake hasa ikizingatiwa kwamba wengi wa Wajumbe ni wapya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2012.   
Mada zitakazowasilishwa kwenye Semina ni pamoja na;
 
1. Nafasi na Wajibu wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa

2. Umuhimu wa Maadili kwa Viongozi na Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi.

3. Mikakati ya kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa nane wa CCM.

4. Mkakati wa kukuza ajira nchini.
 
Semina hii itafuatiwa na Mkutano rasmi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao pamoja na mambo mengine utafanya Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Imetolewa:​

Nape Moses Nnauye

KATIBU WA NEC – ITIKADI NA UENEZI

CHAMA CHA MAPINDUZI



AJALI MBAYA KIBAMBA DARAJANI







 Mwili wa Marehemu Dereva kwa Mbele ukiwa Umekandamizwa na Lori lililo beba Mbao izo
 Huu ni Mguu wa Dereva ambaye amekandamizwa na Gari hilo



 Hivi Ndivyo Gari hili lililo beba Mbao limeanguka

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI HIZI





Baraza la mitahani la taifa leo limetoa tovuti rasmi kwa ajili ya kuangalizia matokeo pindi yatakavyo tangazwa. Tovuti hizo ni www.necta.go.tz na www.matokeo.necta.go.tz. vilevile wamesema kwamba tovuti ya wizara ya elimu www.moe.go.tz haitatumika kwasasa kwasababu haipo hewani.


WABUNGE WATAKAO KATAA KUHOJIWA NA KAMATI WATAKAMATWA NA POLISI

Bunge limesema wabunge watakaokataa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, watakamatwa na polisi na  kufikisha kwenye kikao cha kamati hiyo.

Juiz, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbroad Slaa aliwakataza wabunge wake kuitika wito wa kuhojiwa na kamati hiyo hadi Spika atakapojibu  baadhi ya madai ya chama hicho.

Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, alisema  mbunge anayehitajika kuhojiwa na kamati hiyo hupelekewa barua ya kuitwa na endapo akikataa kufika atakamatwa na  polisi.
“Mbona jambo hili lipo wazi kwa kila mbunge kwa kuwa sheria zinajieleza kuwa ukikataa wito utafuatwa na askari ambaye atakuleta kwa lazima katika kamati hii.
Dk Slaa alikataa wabunge kuhojiwa baada ya  Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuitaka  Kamati ya Maadili  kuchunguza vurugu zilizojitokeza  wiki wakati wabunge walipokuwa wakijadili hoja binafsi ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), iliyohusu upatikanaji wa majisafi na uondoshaji wa majitaka  Dar es Salaam.


HERI YA KUZALIWA MDAU

Kitongoni inachukua fursa hii adhim kumtakia heri ya kuzaliwa mmoja wa wadau wake ndugu Hassan Bilal Kabange ( Abu Khayrat Hassan Kabange)

 





Friday, February 8, 2013

WEMA AONESHA PICHA YA MTU ANAESEMEKANA KUWA MUMEWE

Wema Sepetu akiwa kimahaba na mwanaume aliyedai ni 'mumewe'. Picha hiyo ambayo aliiweka kwenye mtandao wa BBM inamuonesha msanii huyo akibusiana na mwanaume huyo lakini wakionekana kuanzia kwenye kidevu hadi kwenye kiuno kama unavyoweza kujionea mwenyewe hapo.
 
Baada ya kuitupia picha hiyo, Wema aliandika: ‘Miss you mume wangu, wewe ndio kila kitu katika maisha yangu, watasema sana lakini mambo yetu yanatuendea vizuri.” Maneno hayo yanaashiria kuwa Wema anampenda sana mwanaume huyo na si Nasib Abdul 'Diamond' tena.

HATIMAYE MATUMAINI AREJEA DAR NA KUPOKELEWA NA WASANII WENZAKE

    Matumaini (katikati) akisaidiwa na wasanii wenzake muda mfupi baada ya kutua.

 Matumaini (kulia) akiwa na Bi. Mwenda (wa pili kushoto) na anayefuata (kushoto) ni msanii mwenzake Kiwewe wakisubiri gari la kumpeleka hospitali.


    Askari wakiwaelekeza wasanii kukaa upande mmoja ili apate hewa.

 Matumaini akiwa amebebwa mgongoni na msanii mwenzake, Mariam Athuman ‘Kalunde’ akimpeleka kwenye gari.

Mama mkubwa wa Matumaini, Bi. Elizabeth (kushoto) na Matumaini (katikati) wakiwa ndani ya gari tayari kuelekea hospitali ya Amana.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF), Simon Mwakifwamba akizungumza na wasanii maeneo ya Amana wakati Matumaini akiwa kwa daktari.

MSANII wa vichekesho ambaye alikuwa nchini Msumbiji, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ jana alipokelewa na wasanii wenzake kibao baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar akiwa hoi kutokana na kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
Matumaini alitua uwanjani hapo jana majira ya saa 9:30 alasiri ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wasanii walimbeba mgongoni na kumfikisha kwenye gari ambapo walimpeleka moja kwa moja hospitali ya Amana alikolazwa mpaka sasa akiendelea kupatiwa matibabu.


DKT. GHARIB BILAL KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA MAREKANI




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Mazingira, Seneta,Robert D. Hormats, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc Marekani, Feb 6, 2013.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU