Msanii wa Bongo Fleva Q. Chillah
Mapya yanazidi kuibuka kuhusu ushindani wa Diamond na Ali Kiba ambapoushindani huo 
ulianzia katika hitimisho la tamasha la Fiesta lililofanyika katika 
viwanja vya Leaders Club Dar. 
Mashabiki wa wasanii hawa wawili 
wanavutana huku kila mmoja akisema mwenzake ana kipaji na anamfunika 
mwenzake. Inasemekana kuwa kuna baadhi ya mashabiki walikodiwa kwa ajili 
ya kumzomea Diamond wakati akitoa burudani siku ya Fiesta na hilo 
lilithibitishwa na Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond.
kwa sasa katika mziki wa Bongo Flava kumekuwa na fitina nyingi wakati 
mwingine wasanii kwa wasanii wanachonganishwa na mwisho wa siku unakuwa 
ugomvi, kwa mfano sasa hivi bifu la Ali Kiba na Diamond.
Q Chief : "Yote wanayopitia ni changamoto ambazo pengine
 hawakuwahi kuzania kwamba watapitia. Mimi nimepitia situation ambazo 
zimenijenga kuwa "sugu" na "Legendary" ndiyo maana ya kuwa mkongwe unapitia 
situation ambazo watu wengine wanakulazimisha ufike huko. 
Hata kama upo level
 fulani wanakushusha kwa kufikiria kwamba wanaweza kukushusha. Unapandishwa na watu, unapandishwa na mwenyezi Mungu, unashushwa na 
watu, unashushwa na mwenyezi Mungu. 
Mfano niliangalia Fiesta 
kwenye TV sikwenda kwa sababu nilikuwa na mambo yangu Studio, hakuna kitu 
kigeni nlichokiona, nimeona msanii wa marekani anafunikwa na msanii wa 
Tanzania ambaye ni Ali Kiba. 
Nmeona Ali Kiba ambaye amekaa kimya kwa 
miaka mitatu bila Airtime na watu wamemzungumzia vibaya, vizuri na nini 
wamemkubali tena. Ikiwa ni mtu yule yule ambaye wamemkataa na wakumuweka
 mtu mwingine juu. 
Hakuna kitu kisichowezekana, matokeo uliyoyaona juzi 
ndio matokeo yanayotokea na yataendelea kutokea. Hakuna Mungu wa hii 
kazi, hakunaga mfalme wa hii kazi ila kuna masultan wa Hii Kazi. 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
