Baada ya kituo cha Simu 2000 kukamilika SUMATRA kwa kushirikiana na 
Manispaa ya Kinondoni na Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni
 tumekubaliana kufungua kituo hiki tarehe 23.10.2014 asubuhi, kwa 
daladala ambazo zilikuwa zinaishia au kuanza safari katika kituo cha 
daladala Ubungo.
Kila dereva anatakiwa kufuata utaratibu ulioelekezwa hapa chini ili kuondoa usumbufu usio na tija.
1. DALADALA ZINAZOTOKA MASAKI
zikifika
 barabara ya Shekilango zitaingia  kulia kwa kutumia barabara ya TANESCO
 inayokwenda moja kwa moja kituoni simu 2000 na zitarudi barabara ya 
Shekilango kwa kutumia  njia hiyo hiyo ya TANESCO.
2. DALADALA ZINAZOTOKA KARIAKOO, POSTA na KIVUKONI
zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kulia (barabara ya Sam Nujoma) kwenda
 kituoni Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo
3. DALADALA ZINAZOTOKEA BARABARA YA MANDELA
zitavuka
 mataa ya Ubungo (kwa kutumia barabara ya Sam Nujuma) na kwenda kituoni 
Simu 2000, zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.
4. DALADALA ZINAZOTOKEA MWENGE
zikikaribia
 jengo la  Mawasiliano Towers zitachepukia kushoto kwa kutumia service 
road inayopita mbele ya Mawasiliano Towers  hadi kituoni simu 2000, 
zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara ya Sam Nujoma (sio servive 
road).
5. DALADALA ZINAZOTOKEA KIMARA NA MBEZI
zikifika mataa ya Ubungo zitaingia kushoto kwenda kituoni simu 2000. zitarejea zilikotoka kwa kutumia barabara hiyo hiyo.
Conrad Shio
Afisa Mfawidhi SUMATRA –DSM
0755 660 016
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog