Facebook Comments Box

Wednesday, October 8, 2014

JK KUPEWA KATIBA MPYA LEO



Stori:  Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea ‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete
Bunge hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya katiba mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba inayopendekezwa iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.

Katiba hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi mbalimbali yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga. 
GPL.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU