Bodi ya ligi kuu
soka Tanzania bara TPL Bord imemtangaza mchezaji  wa Azam FC Salum Abubakar  ‘Sure 
Boy’ kuwa mchezaji bora wa mwezi oktoba katika ligi kuu soka Tanzania
Bara.
Akizungumza leo
Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Bodi ya ligi, Mkurugenzi wa Masindano wa TFF
Boniface Wambura amesema mchezaji uyo amechaguliwa baada ya kuwasinda kwa
vigezo wachezaji wenzake katika michezo ya mwezi  uu wa oktoba.
Mwezi  uliopita 
mchezaji  wa Mbeya City Antony
Matogolo aliibuka  mchezaji bora wa 
mwezi  septemba na kuambulia  kitita cha shilingi milioni moja. 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
