Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo 
wa mpira wa vikapu  imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia  
yanayofanyika huko Korea Kusini baada ya kuagizwa kuvua  hijab kabla ya 
 mechi yao dhidi ya timu ya Mongolia .
Wanawake hao walikataa kata
 kata kuvua  vazi hilo na wakajiondoa mashindanoni wakidai inakiuka 
maagizo ya dina ya Kiislamu inayomtaka mwanamke kujistiri nywele zake 
haswa akiwa faraghani.
Sheria za shirika la mchezo huo duniani 
haziruhusu kuvaliwaj  kwa  vitambaa vya kichwani  wakati wa mechi lakini
 sasa wamekuwa wakijadili iwapo sheria hiyo itaondolewe.
Hata 
hivyo ilipowadia wakati wa mechi yao dhidi ya Nepal sheria hiyo haikuwa 
imebadilishwa na hivyo iliwabidi kuyaaga mashindano. 
Fani nyengine za michezo katika mashindano hayo ya Bara Asia zinaruhusu uvaliwaji wa hijab.
Timu ya taifa ya unyanyuaji uzani ya Iran imekuwa ikishiriki mashindano hayo huku wakiwa wamevalia hijab.
Baraza la mashindano ya Olimpiki ya Bara asia OCA imesema kuwa haki za wachezaji ni zinapaswa kupewa kipaombele .
Baada ya kuyaaga mashindano hayo mchezaji wa Qatar Amal Mohamed A 
Mohamed alisema kuwa walikuwa wamehakikishiwa kuwa wataruhusiwa 
kushiriki mashindano hayo wakiwa wamevalia hijab na hivyo hawaelewi 
kwanini sheria hiyo haijabadailishwa.
''nina hakika kuwa hatutashiriki mashindano yeyote ya Bara Asia hadi sheria hiyo ibadilishwe''
Mashindano
 hayo hufanyika kila baada ya miaka 4 na huwaleta pamoja washiriki 9000 
kutoka mataifa 45 yakishindana katika fani 36 ya michezo.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 4 Oktoba. 
Chanzo: BBC 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog

