| Kocha Abdulghani Msoma na kocha msaidizi Rashid Lato wakiwafatilia kwa karibu vijana wa Malindi. | 
 Klabu  ya  malindi 
ya  mjini  Unguja  imeliongezea  makali 
benchi  lake  la 
ufundi  lililokuwa  likiongozwa 
na  Mohamed  Said 
Shubery  al  maarufu 
Babu  Shube  na  badala 
yake  sasa  litakuwa 
likiongozwa  na  makocha  watatu  na  si
wawili tena  na  wamemuongeza  kocha 
Abdulghani  Himid  Msoma 
katika kuinoa  timu hiyo  inayoshiriki 
ligi  kuu  ya 
Zanzibar  inayofahamika  kama 
Grand malt  premier  league.
Uamuzi  huo  wa  malindi  umekuja  kufuatia 
matokeo  mabaya 
waliyopata  katika  mechi 
zao  mbili  za ligi 
walizocheza  na  mpaka 
sasa  kuwa  hawana 
hata  point  moja  ila  wameambulia 
magoli  mawili  tu  uongozi 
umeamua  kumuongezea  nguvu 
za  kiufundi  kocha 
huyo  mwenye  maneno 
mengi  mfano  wa 
kocha  Chelsea  ya 
Uingereza  Jose  Mourinho, Mohamed  Shubery 
au  Babu. Leo 
asubuhi  alionekana  yuko 
samba samba  na  kocha 
Msoma na  pamoja  na 
msaidizi wake  Rashid  Lato katika mazoezi ya mwisho Katika  uwanja 
wa  Amaan  kabla 
ya  mchezo  wa leo.
 Kocha   Msoma 
aliyeanza  kazi  hiyo 
ya  kuwanoa  Malindi 
juzi  asubuhi  Kwenye 
uwanja  wa  Amaan 
na  jana  kuendelea  na 
mazoezi  hayo  asubuhi 
mtihani wake  wa  kwanza 
ulikuwa   ni  leo  ambapo 
Malindi  ilishuka  dimbani 
kupepetana  na  timu 
ya  Polisi  ya 
Zanzibar  kwenye  uwanja 
wa  Amaan  katika 
mchezo  uliochezwa  saa 
10  Alaasiri  umeshuhudiwa 
Malindi  ikiibuka  na  
ushindi  wa  goli 
moja  kwa  nunge 
dhidi  ya  maafande 
hao  Polisi  Zanzibar, Malindi  sasa 
baada  kuonja  ushindi 
huo  hii  leo 
angalau  sasa  wana 
point  tatu  na 
magoli  matatu.
| .Malindi wakiwa katika mazoezi jana asubuhi ktk uwanja wa Amaan. | 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog