Simba 
 Yanga
Timu
 ya yanga  inatarajiwa  kutua  mjini  unguja  Zanzibar  hapo  kesho  
ikitokea Pemba ilikokuwa  imeweka  kambi  yake ya wiki moja, timu  hiyo 
 yanga itacheza mechi mbili tu  za  kirafiki  mjini hapo ambapo  
mechi yake  ya  kwanza  inatarajiwa kuwa  siku ya juma pili  jioni  
itakapo pambana na timu  ya Shangani  FC.
Wakati huo kocha wa timu  
hiyo Maximo  amewaomba  radhi  wana yanga wa mjini  Pemba  kwa  
kutokucheza na timu ya Coastal  Union kwa kile  alichoita  kuwa 
haikuwa  kwenye  program  yao na pili muda wao umekwisha  kwa kuwa 
walipanga  kucheza mechi moja tu kisiwani pemba na mechi  2 Unguja.
Na baada  ya hapo  
wataenda  Dar es salaam kucheza mechi moja ya kimataifa, lakini kocha 
huyo aliwapongeza wana yanga hao kwa kuwa  bega kwa bega na timu yao 
kwa kipindi chote  ambacho timu hiyo  ilikuwa visiwani humo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog

