Na Mwandishi Wetu
 
SURA ya Tanzania inazidi kuchafuka katika suala la usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba (jina tunalihifadhi kwa sasa), kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege.
 
SURA ya Tanzania inazidi kuchafuka katika suala la usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba (jina tunalihifadhi kwa sasa), kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege.
Mshambuliaji 
huyo aliyewahi kuichezea Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000, amekamatwa na
 madawa ya kulevya siku tatu zilizopita kwenye Uwanja wa Ndege wa 
Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia.
 
Vyombo vya habari 
vya Ethiopia vimetangaza kukamatwa kwa wanamichezo wawili, mmoja 
akijitambulisha ni mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa, Taifa 
Stars.
 
Taarifa hizo zimeeleza kwamba wachezaji hao walikamatwa baada
 ya kutua Bole wakitokea Burundi na wote wawili walikuwa na pasi za 
kusafiria za Tanzania.
 
Huenda waliamua kupitia Bujumbura ili kukwepa
 ukali wa ulinzi ulioboreshwa kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa 
Julius Nyerere (JNIA) baada ya Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe 
kutaka mambo yawe hivyo na kulivalia njuga suala la madawa ya kulevya.
 
Mwanamichezo mwingine alielezwa kuwa aliwahi kuwa bondia. Taarifa hizo 
zimeeleza mwanasoka wa zamani wa Simba alikamatwa wakati akipanda ndege 
kutoka Addis Ababa kwenda Zurich, Uswiss ambako angepanda treni kwenda 
Stockholm, Italia anakoishi.
 
Championi Jumatatu liliamua kufuatilia 
zaidi kwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya
 Tanzania, Godfrey Nzowa aliyesema yuko nje ya nchi kikazi lakini 
akaahidi kulishughulikia suala hilo.
 
“Niko nje ya nchi kikazi, sina 
taarifa na suala hilo zaidi ya ile meli iliyokamatwa Italia na madawa na
 imesajiliwa Tanzania. Lakini nitalifanyia kazi, nipe muda nilikabidhi 
kwa Interpol na watalifanyia kazi,” alisema.
 
 Lakini Mtanzania 
mwingine anayeishi nchini Italia alisema kuna taarifa za kukamatwa kwa 
mwanasoka Mtanzania ambaye anaishi nchini humo.
 
“Tumeambiwa ni 
(anamtaja), unajua sasa alikuwa hachezi soka na taarifa zimezagaa eneo 
kubwa la Stockholm. Lakini bado hatujawa na uhakika.
 
“Huyo 
mwanamichezo mwingine (anamtaja), alikuwa na mke Mzungu hapa na 
amepigiwa simu kwamba mumewe amekamatwa. Sasa tunaendelea kusubiri 
uthibitisho kuhusiana na hilo,” alisema Mtanzania huyo ambaye ameishi 
Sweden kwa zaidi ya miaka sita sasa.
 
Juzi na jana, taarifa za 
kukamatwa mwanamichezo mwingine bondia Mbwana Matumla katika mpaka wa 
Ujerumani na Uswiss akiwa na madawa zilizagaa.
 
Kamanda Nzowa pia 
alisema analifuatilia hilo lakini kaka mkubwa wa bondia huyo, Rashid 
Matumla alisema suala hilo halina uhakika.
 
“Nimekuwa nikimtafuta 
Mbwana kwenye simu kwa zaidi ya siku kumi bila mafanikio, ukweli hatuna 
uhakika na suala hilo na tunaendelea kulifuatilia.
 
“Napenda tupate 
uhakika kwanza, ninawashauri watu kuacha kusema moja kwa moja kama ni 
kweli hadi tutakapopata uhakika kwa kuwa sijampata kwenye simu hadi 
sasa,” alisema Matumla.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa, mwanasoka huyo aliyenaswa alikuwa jijini Dar siku chache zilizopita na kuonyesha kufuru ya fedha baada ya kutumia zaidi ya shilingi milioni mbili kuwatuza wanamuziki wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ katika onyesho lake moja jijini humo
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa, mwanasoka huyo aliyenaswa alikuwa jijini Dar siku chache zilizopita na kuonyesha kufuru ya fedha baada ya kutumia zaidi ya shilingi milioni mbili kuwatuza wanamuziki wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ katika onyesho lake moja jijini humo
.CHANZO GPL
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
