Mrembo
 Severina Lwinga juzi alifanikiwa kuwa mrembo wa tano kuingia nusu 
fainali ya shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 baada ya kutwaa taji la
 Miss Personality 2013. Mshindi wa taji hilo anapatikana kwa kupigigiwa 
kura na warembo wenzake.
Severina ameungana na Miss
 Tanzania Photogenic
2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, 
Miss
Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports 
Woman, Clara
Bayo kuingia katika nusu fainali ya Miss Tanzania ambayo itafanyika 
Jumamosi hii ukumbi wa Mlimani City. Shindano hilo lilifanyika Mgahawa 
wa AK'S ulipo mtaa wa Samora. 
 Warembo
 walioingia tano bora ya Miss Personality 2013 shindano lililofanyika 
katika magahawa wa AK'S uliopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Warembo watano ambao wamefanikiwa kuingia hatua
ya nusu fainali ya Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara
jana. Kutoka kushoto  ni Miss Tanzania Photogenic
2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania
Personality, Severina Lwinga, Miss
Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara
Bayo.
  
 Warembo wakiwa ndani ya mgahawa wa AK'S jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi
 wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa 
Miss Tanzania akiwa na Mkurugenzi wa Mgahawa wa AK'S, Kishan. 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog