Aliyewahi kuwa mgombea wa Uchaguzi Mkuu Shirikisho la Soka 
Tanzania (TFF) uliosimamishwa na Fifa, Michael Wambura, amesema 
hatashiriki tena kwenye uchaguzi ujao wa shirikisho hilo, Oktoba 27.
Awali Wambura, aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT 
(sasa TFF), aliwania nafasi ya Makamu Rais katika uchaguzi 
uliosimamishwa na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), kutokana na 
kuwepo malalamiko kutoka kwa watu  walioenguliwa akiwamo yeye.
Jana TFF ilitangaza majina ya wagombea 58 wote 
ikiwa ndiyo siku ya mwisho  kurejesha fomu, lakini bila kuwepo kwa jina 
la Wambura ambaye  alipoulizwa na Mwananchi sababu ya kutogombea tena 
alisema: “Siwezi  kujisafisha na majitaka.”
“Nimeamua kupumzika, nilipigania haki imepatikana 
kwa kamati mbili kuundwa. Bila mimi kamati hizo zisingekuwapo, lakini 
jambo muhimu ni kwamba siwezi kujisafisha na majitaka,” alisema Wambura.
“Mfumo wa uongozi TFF ni mbovu, kumejaa siasa za 
majitaka, hizo kamati  zilizoundwa hazitafanya kazi kwa vile tu Wambura 
hayupo, ningekuwepo  zingepata kazi ya kufanya,” alitamba Wambura.
Nafasi ya Makamu wa Rais inawaniwa na Iman Madega,
 Ramadhan Nasib na  Walace Karia, huku wajumbe waliomba kuwakilisha 
kanda mbalimbali ni Abdallah Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Magati, Mugisha
 Galibona, Vedastus  Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra  Swai, Mbasha 
Matutu, Stanslaus Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Mbise na Omari Walii. ni 
Ahmed Mgoyi, Yusuf Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius 
Kilungeja, Ayoub  Nyenzi, Cyprian Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala,
 Eliud Mvela, John  Kiteve, James Mhagama, Kamwanga Tambwe na Stanley 
William Lugenge, Athuman Kambi, Francis Kumba, Zafarani Damoder.
Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Masima, 
Farid Nahdi, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Riziki Majala, Twahil Twaha 
Njoki, Davis  Mosha na Khalid  Mohamed. Alex  Kamuzelya, Juma Pinto, 
Muhsin Balhabou, Omar Abdulkadir, Shaffih Dauda na Wilfred  Kidao. Kwa 
upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili Hamad
 Yahya (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).Walioomba 
nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Muzo, Michael  Kaijage, Omari 
Mwindadi, Salum Rupia na Silas Magunguma.
CHANZO:SHAFFIH DAUDA 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog