
 Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaah wa Barakaatuh, 
 Tunapenda
 kuwaarifu kuonekana kwa mwezi mpya wa Shawwaal leo hii Jumatano (07 
Agusti 2013M). Kwa hiyo, kesho Alkhamiys In Shaa Allaah ni tarehe 1 
Shawwaal 1434H (08 Agusti 2013M) na ndio Siku kuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.
 Kwa
 Munaasabah huu wa ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda kuchukua fursa hii 
kuwasilisha salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, 
tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na 
zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM’
 (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi 
wanapokutana katika siku ya 'Iyd). Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na 
Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama
 na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.
 Mwisho,
 bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu Waislam wote waliopo kwenye 
dhiki, vita, ukandamizwaji, njaa, maradhi na wanaodhulumiwa pote 
duniani. Tukimuomba Allaah (Subhaanahu wa ‘Ta’ala) Awakwamue na kuwapa 
faraja na nusra. 
 Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn
 Tafadhali bonyeza kwenye picha ifuatayo upate Takbiyrah ya 'Iyd

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog