Msaani mwenye kipaji cha 
Hali ya juu nchini na Mwenye umri mdogo Elizabeth Michael 
"Lulu"anatarajia kuzindua filamu yake ya Kwanza tangu atoke 
Gerezani, Filamu hii iitwayo FOOLISH AGE ikiwa imetengenezwa na Kampuni ya
 Proin Promotion Limited itazinduliwa Mnamo tarehe 30 August 2013 Katika
 Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar Es Salaam. 
Filamu hiyo inayoelezea 
Maisha ya Lulu ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu 
kutokana na Kutengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion Limited Katika 
Uzinduzi huo wa Filamu hiyo, Wasanii mbalimbali akiwemo 
mwanamuziki Lady Jaydee na Machozi  Band wanatarajiwa kushusha burudani kabambe.
Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa  kijamii(facebook) Lulu aliyejaaliwa kuwa na kipaji cha kuigiza na mwenye 
mvuto mbele ya runinga aliandika "Nina  kila sababu ya kumshukuru 
Mungu, napenda kuwafahamisha kuwa  TAREHE 30/8/2013 ndio siku
 nitakayozindua movie yangu mpya iitwayo FOOLISH  AGE....Hatimaye narudi
 kazini. 
 Baada ya uzinduzi wa Filamu hii nakala zitaendelea kuuzwa katika maduka
 yote ya Filamu nchini, Usikose uzinduzi Huu utakaofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City tarehe 30 August 2013.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
