Bi Denisia Mangwea.mama mzazi wa msanii Albart Mangwea
 Mama mzazi wa  marehemu Albart Keneth Mangwea 'NGWEA' Bi Denisia 
Mangwea[63] leo asubuhi ameanguka ghafla baada ya kupokea taarifa kwamba
 mwili wa mtoto wake Albeth umeshindwa kuwasili nchini ukitokea Afrika 
ya kusini.Mtandao huu leo mchana ulipokea taarifa z a tukio hilo  
ambapo dada mkubwa wa Albeth Bi Magreth Mangwea alipoulizwa 
alithibitisha mama yake kuanguka ghafla baada ya kusikia mwili wa 
mpendwa mtoto wake umeshindwa kuwasili  nchini.
" Ni kweli leo asubuhi mama alipoamka na kusikia taarifa kuwa mwili wa mwanae hautofika tena leo Jijini Dar es Salaam kutokana na Taarifa ya Daktari kuchelewa kutolewa 
 alianguka kwa presha na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro 
akiendelea na matibabu, na alizinduka baadae  na anaendelea 
vizuri na kwamba muda wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo. 
 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog