![]()  | 
Idd Simba | 
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, hivi punde  
imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es  
Salaam (UDA), Idd Simba, Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani 
wa  Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda, Meneja Mkuu wa shirika hilo 
Victor  Milanzi
 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa 
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo kwa sababu  
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya  
kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya  
kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka  
2002. 
Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama,matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi.
Hivyo kuanzia sasa washitakiwa hao wapo huru
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
