Mkuu wa Mkoa Mulongo naye 
amefika  eneo  la 
tukio  na  kuwafariji 
wahanga  wa  tukio 
la  bomu....
RPC  wa  mkoa 
wa  Arusha  naye aliambatana  na 
mkuu  wa  mkoa 
na  muda  huu 
alikuwa  anatoa  nasaha 
zake  kwa  wananchi....
RPC  amesema  tukio 
hili  ni  la kigaidi. Amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa
kujificha na kurusha bomu. ...
Amesema kuwa Polisi wanawasaka waliohusika  na 
unyama  huu  na 
ameomba yeyote  mwenye taarifa
yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako 
mahututi
Mpaka sasa  mtu mmoja
anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi
 INASEMEKANA KUWA BOMU LIMELIPUKA KATIKA KANISA KATOLIKI PAROKIA MPYA YA OLASITI ILIYOKUWA INAZINDULIWA LEO JIJINI ARUSHA MUDA HUU.
BOMU HILO LIMELIPUKA WAKATI 
WAUMINI WA KANISA HILO LA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA
 KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA  NA MPAKA SASA  HAIJAWEZA KUJULIKANA 
IDADI KAMILI YA WATU WALIOJERUHIWA LAKINI TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA 
BAADHI YA WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU
 NA MPAKA MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BOMU HILO 
KULIPUKA.
Mh Zitto Kabwe alizungumzia hilo katika ukuta wake wa facebook 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog