Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kubwa 
  |  
| Waumini
 wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kusikiliza hukumu ya kesi ya 
Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja ya muumini mwenzao ambae alishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo 
kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. |  
 
 
HATIMAYE katibu
 wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na 
wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu 
jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa 
yakiwakibili. Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka
 mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa
 hilo. 
Mara
 baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za 
furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na 
eneo la Mahakama hiyo. 
Pamoja
 na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo 
mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao. 
1.Mahakama
 hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na 
masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua 
kuna tatizo umiliki. 
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa. 
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria. 
4.Hakimu
 awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai 
mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa. 
5.Upande
 wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya 
mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu 
za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni 
yaliyokusudiwa. 
 
 
  |  
| Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu. |  
 
  
  |  
| Tumewashinda! |  
 
 
 
 
 
 
  |  
| Furaha! |  
 
  |  
| Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda! |  
 
 
 
  |  
| Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza. |  
 
  |  
| Hoyoooooooooo! |  
 
 
 
  |  
 
 
Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia ndugu yake kutokana na kushinda kesi hiyo. 
 |  
 
  |  
| "Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia. |  
 
 
 
  |  
| Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia! |  
 
 
 
  |  
 
 
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea. 
 |  
 
  |  
 
 
Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao. 
 |  
 
  |  
| Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa. |  
 
 
  |  
| Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu! |  
 
 
 
 
 |