Mbunge
 wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu (CHADEMA) akitoka Mahakamani na
 mawakili wake Humphrey Mtui na Method Kimomogoro asubuhi hii mara baada
 ya kesi inayomkabili kuahirishwa 
Hakimu
 Devota Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ameahirisha hadi Julai 
7, 2013, shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, 
Godbless Lema (CHADEMA), kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi wa Chuo 
cha Uhasibu Arusha (IAA) anaotuhumiwa kuufanya Aprili 24 mwaka huu, ili 
kesi hiyo ianze kusikilizwa upelelezi utakapokuwa umekamilika.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog