Askari 
mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha kudhalilishwa kijinsia na wanawake
 wanne kwa wiki moja kabla ya kupigwa mawe na kutupwa katikati ya
 milima huko Zimbabwe. Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini nchini humo,Wanawake 
wawili na mwanaume mmoja walikuwa kwenye gari, Mercedes Benz, na baada 
ya kuendesha kwa takribani saa moja kuelekea mji huo, dereva wa gari 
hilo akabadili mwelekeo wa safari hiyo.
Msemaji wa polisi wa Manicaland,
 Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa 
mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na 
walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula. Askari 
huyo alitaka kushushwa, lakini dereva huyo akatoa kisu na kumtishia 
nacho. Mmojawa abiria wanawake akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni 
mtuhumiwa huyo."
 Kwa 
mujibu wa Nuzondiwa,watesi  hao walimpeleka mlalamikaji kwenye nyumba 
isiyojulikana ambako walimvua nguo zote na kumpora simu yake na Dola za 
marekani 35.
 Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya Aprili 19-23. Kisha 
akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye Milima ya Dangamvura
 ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika mguu wake wa 
kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
 Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Sakubva.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
