Timu zinazoshiriki ligi kuu ya 
England zinatarajiwa kukubaliana kupitisha matumizi ya teknolojia  ya 
mstari wa Goli maarufu kama GOAL LINE TECHNOLOGY baadaye wiki hii ambapo
 taarifa toka kwenye chama cha soka cha England imesema kuwa klabu hizo 
zimezungumzia suala la matumizi ya teknolojia hiyo na zitakutana tena 
siku ya alhamis ambapo agenda kuu ya mkutano huo inatarajiwa kuwa 
makubaliano ya kupitisha matumizi ya teknoljia hiyo kwenye michezo ya 
ligi kuu ya England kuanzia msimu ujao.
Kampuni ambazo zimeingia kwenye
 mashindano ya kuwania tenda ya ufungaji wa teknolojia hiyo kwenye 
viwanja vya ligi kuu ya England ni Kampuni ya HawkEye,Cairos,Goalcontrol
 na Goalref ambapo teknolojia hiyo itaanza kutumika kwenye mchezo wa 
ufunguzi wa ligi kuu ya England ambao ni mchezo wa kuwania Ngao ya jamii
 unaochezwa kati ya mshindi wa ligi kuu na mshindi wa kombe la Fa, 
tayari shirikisho la mchezo wa soka ulimwenguni FIFA limepitisha 
matumizi  ya Goal line Technology ambapo teknolojia hiyo itaanza 
kutumika kwenye michuano ya kombe la mabara.
Chama cha soka cha England 
tayari kimepitisha matumizi ya teknolojia hiyo kwenye uwanja wake wa 
Taifa wa Wembley na kimeanza kupitia mapendekezo mbalimbali toka kwenye 
makampuni yanayofunga mifumo ya teknolojia hiyo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog



